Njombe

Watu wawili ambao ni mume na mke wamefikishwa mahakamani katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa Njombe wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa makosa matatu likiwemo la kuuza mbolea feki iliyowekwa katika mifuko 221 ya mkampuni mbalimbali na kuuzwa kwa wakulima zaidi ya 58 .

Akisoma mashtaka yao ya kesi namba moja ya uhujumu uchumi ya mwaka 2023 wakili wa serikali kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka mkoa wa Njombe Matiku Nyangero amewataja watuhumiwa kuwa ni Benedict Ereneus Masasi na Faraja Jumanne Sago wakazi wa mtaa wa Mjimwema mjini Njombe wanatuhumiwa kwa makosa matatu ya uhujumu uchumi.

Amesema kosa la kwanza ni kuuza mbolea feki kinyume na kifungu cha sheria cha 40 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili cha sheria ya mbolea no ya mwaka 2009

Kosa la pili ni kula njama ya kutenda kosa kinyume na kanuni ya paragraph ya 4kifungu cha kwanza a cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya 2022

Na kosa la tatu ni kuisababishia hasara mamlaka ya kudhibiti mbolea tanzania tfra kinyume na kanuni ya paragraph ya 10 kifungu cha kwanza ya jedwali la kwanza la kifungu cha 57 na 60 cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 iliyofanyiwa marejeo mwaka mwaka 2022

Nyangero amesema makosa hayo yalitendeka kati ya mwezi 11 mwaka 2022 hadi January 2023 maeneo ya mitaa ya Mgodechi na Ramadhani ndani ya wilaya na mkoa wa Njombe ambapo pia imeelezwa kuwa wastakiwa walikuwa wakiuza mbolea za ruzuku zilizopunguzwa ujazo.

Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Njombe Liad Chamshama amesema kuwa washtakiwa hawatajibu chochote kutokana na mahakama kutokuwa na malaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Katika kesi hiyo inayotetewa na mawakili wawili ambao ni Musa Mhagama na Osca Mwenda washtakiwa wamepata kwakuweka bondi ya shilingi milioni 30 ya mali zisizo hamishika ambapo wao wawiwili wameka bondi ya shilingi milioni kumi kila mmoja na wadhamini wao wawili wameweka dhamana ya shilingi milioni tano kila mmoja na wako nje kwa dhamana kwa mujibu wa wa sheria kifungu cha 29 kifungu cha 4 cha makosa ya uhujumu uchumi na wamepewa dhamana mpaka hapo march 30 mwaka huu kesi itakapo tajwa tena.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...