Na Karama Kenyunko Michuzi TV


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu kesho Machi 15, 2023 inatarajia kuwasomea adhabu wanandugu watatu baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kuwashambulia na kuwadhuru mwili Rashid Mohamed na mpenzi wake Anitha Rauyan wakidai wamewakamata ugoni

Washtakiwa hao, Singbard Buchard, Albert Buchard na Delfina Buchard wametiwa hatiani leo Machi 14, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi wakati kesi yao ilipoitwa kwa ajili ya kusomwa.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Kyaruzi Evodia amesema washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni shambulio la kudhuru mwili na kusababisha majeraha ya hatari na kudhuru mwili.

Hakimu Evodia amesema, amepitia ushahidi wote uliotolewa na upande wa Jamuhuri na ule wa utetezi na kwamb , mahakama imewakuta na hatia kwa shtaka la moja la la shambulio la kudhuru mwili.

Amesema, mahakama imeridhika kwamba washitakiwa wote ndiyo chanzo cha walalamikaji kujeruhiwa na hivyo wanatiwa hatiani.

"Washitakiwa wote ni wanandugu, walifika eneo la tukio na walihusika kuwashambulia walalamikaji, wote walionekana kuwa na nia moja, waliwavamia na kuwapiga na ushahidi huo unaungwa mkono na matabibu waliowahudumia " amesema Hakimu Evodia"

Alisema washitakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo Julai 29 mwaka 2021 eneo la Voda, Kongowe, wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa, Mohamed na Anitha ni wapenzi ambapo siku ya tukio, washitakiwa waliwavamia wakiwa chumbani.

Ilidaiwa kwamba, waliwavamia kwa madai kwamba Mohamed alikuwa anatembea na Anitha ambaye alikuwa mke wa Singbard (mshtakiwa wa kwanza).

Inadaiwa kuwa baada ya uvamizi huo, washtakiwa hao waliwapiga Mohamed na Anitha sehemu mbalimbali za mwili , kwa kutumia fimbo, waliwafunga mikono na kisha kuwapeleka kwa kiongozi wa eneo hilo wakiwatuhumu kwa ugoni.

Katika utetezi wao, washtakiwa hao walikana kuhusika kuwadhuru Mohamed na Anitha, huku wakikiri kufika eneo la tukio.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...