Na Karama Kenyunko Michuzi TV
ALIYEKUWA Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Lydia Ngua na wenzake wanne, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la wizi wa Sh. 600,000/-
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Shaban Hamis, Shukuru Mwagu, Mpelembe Mpelembe na Thaa Mwagu wote wakazi wa Dar es salaam.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Caroline Matemu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Amir Msumi imedai Februari 21, 2022 washitakiwa wote kwa pamoja wakiwa eneo la Charambe Kisutu wilaya ya ilala jijini Dar es Salaam waliiba fedha takwimu Sh. 600,000 mali ya Sophia Mbaga.
Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana yaliyomtaka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya shilingi milioni moja.
Kwa mujibu wa upande wa Jamuhuri upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na imeahirishwa hadi Machi 23,2023 itakapokuja kwa ajali ya washtakiwa kusomewa maelezo ya wali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...