Na Khadija Seif, Michuzi Blog

KUELEKEA kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani,Kampuni ya usafirishaji ya Silent Ocean imetangaza muendelezo wa mashindano ya Ramadhani Cup yatakayoanza wiki ijayo yakilenga kuibua kwa vipaji kwa Wakazi wa Jiji la Dar es Salama.

Akizungumza na waandishi wahabari Leo Machi 16,2023 Meneja Masoko wa Kampuni Usafirishaji Mizigo ya Silent Ocean Mohammed Kamilagwa amesema kuwa mashindao hayo yatashirikisha timu 20 kutoka taasisi mbalimbali yatafanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park kwa siku 29 huku michuano hiyo ikifafitwa kupangwa kwenye makundi matani kwa timu shiriki.

"Tumebakiza siku chache kuingia kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa upande wetu simba wa bahari tunatumia mwezi huo kudumisha undugu,mshikamano na umoja wetu imepelekea tuone michezo ina nafasi kubwa sana katika kuweka watu pamoja".

Mashindano ya Ramadhani Cup ni ya awamu ya nne kufanyika huku kampuni ya Silent Ocean kwa mwaka huu ikiwa ni mara yao ya kwanza kudhamini na kuandaa shindano hilo.

Hata hivyo ameeleza kuwa Timu hizo zitakazoshiriki Ligi hiyo zitahusisha taasisi mbalimbali ambazo zitakuwa tayari kujaza fomu za ushiriki wao makao makuu ya ofisi za Silent Ocean Lumumba Jijini Dar es salaam na Mashindano hayo yatarushwa mubashara Azam tv ambapo kwa sasa zawadi haijawekwa wazi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Usafirishaji Mizigo Silent Ocean akizungumza na Wanahabari Leo Machi 16,2023 Jijini Dar es salaam wakati akitambulisha Mashindano ya Ramadhani Cup yatakayoanza wiki ijayo yakilenga kuibua vipaji na kuwaleta karibu wadau wa kampuni hiyo huku Mashindano hayo yakishirikisha taasisi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...