Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
Imrelezwa kuwa matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea imekuwa kikwazo katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mimea nchini.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma leo Machi 1,2023 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru wakati akielezea majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.
Prof.Ndunguru amesema kuwa Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea.
“Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu changanya na Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea,”amesema Prof.Ndunguru
Aidha Prof.Ndunguru, ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi na inaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.
“Madhara ni mengi ndio maana tulitilia mkazo kwa kuwajengea uelewe wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu sababu wanapopulizia viuatilifu visivyosahihi vinawajengea usugu wadudu waharibifu na kuuwa wadudu rafiki wa mimea,” amesema Prof.Ndunguru
Akitoa takwimu za Uchambuzi wa sampuli mbalimbali zilizofanywa na Mamlaka hiyo ,Prof.Ndunguru ameeleza kuwa sampuli 1025 za viuatilifu (analysis of pesticide samples) ambazo zimeshafanyika ikiwa sampuli 1005 sawa na asilimia (98.04%) zilikidhi viwango huku sampuli 20 (1.96%) zimeonesha kutokidhi viwango.
Na kusema kuwa Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji
198 vilisajiiliwa huku Vibali vya shehena za viuatilifu 1324 vyenye ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 ambapo Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu.
''Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vilisajiiliwa Vibali vya shehena za viuatilifu 1324; ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...