Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) imezindua rasmi mradi wa Boresha Habari ili kuhakikisha kwamba Waandishi chipkizi wa Vyuo vikuu na vyuo vya kati wanakuwa na uelewa hasa kwenye usawa wa kijinsia wakati wa uandishi pamoja na kuripoti habari zenye mlengo wa kijinsia baada ya kuhitimu Masomo yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Deo Temba amesema tutahakikisha waandishi hawa wa habari ambao bado hawajaingia kwenye vitendo wanaelewa vizuri masuala yote ya usawa wa Kijinsia pamoja na kujua uandishi wa habari wa Kijinsia pamoja na kujua jamii kwa ukaribu zaidi hasa wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu.
Pia amesema lengo ni kuona waandishi hao wanaandika makala au habari zinazohusiana na masuala yenye mlengo wa Kijinsia hawa kwa kuweka kwenye mitandao ya kijamii ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
“Bila kuwa na waandishi wa habari wazuri wanaojua masuala ya usawa wa Kijinsia hatuwezi kuwa na maendeleo mazuri hivyo uzinduzi wa mradi huo kwenye Chuo cha Practical School of Jounalism ili kuanza mafunzo kwenye chuo hicho yanayohusiana na Masualayenye mlengo wa Kijinsia." Alisema Temba
Mtangazaji wa Clouds TV, Sakina Lyoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari ili kuhakikisha kwamba Waandishi chipkizi wa Vyuo vikuu na vyuo vya kati wanakuwa na uelewa hasa kwenye usawa wa kijinjisia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani uliofanyika katika Chuo cha Practical School of Jounalism kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu masuala ya usawa kijinsia kwa wanafunzi wa Chuo cha Practical School of Jounalism kwenye uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari uliofanyika katika chuo hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Mratibu wa Mradi wa Boresha habari Mariam Oushoudada akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wa chuo cha Practical School of Jounalism wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Esther William akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja pamoja na maswali yaliyokuwa yanaulizwa wakati wakati wa uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari ili kuhakikisha kwamba Waandishi chipkizi wa Vyuo vikuu na vyuo vya kati wanakuwa na uelewa hasa kwenye usawa wa kijinjisia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Practical School of Jounalism akitoa nenso la shukrani kwa uongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kuweza kuzindua mradi wa Boresha Habari ili kuhakikisha kwamba Waandishi chipkizi wa Vyuo vikuu na vyuo vya kati wanakuwa na uelewa hasa kwenye usawa wa kijinjisia katika chuo hicho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wakufuatilia mada kwenye uzinduzi wa mradi wa Boresha Habari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...