Njombe
WANANCHI wa kata ya Kifanya halmashauri ya mji wa Njombe wanadaiwa kuficha taarifa za vifo vya wapendwa wao wanapofariki nyakati za jioni au usiku ili kuepuka gharama za kusafirisha miili zaidi KM 50 mpaka Mochwari iliyopo hospitali ya mji wa Njombe Kibena.

Hayo yamebainishwa kwenye mdahalo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za mradi wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya jamii kwenye sekta ya afya (PETS) unaofadhiliwa na shirika la foundation for Civil Society unaotekelezwa na shirika la Highland Hope Umbrella (HHU) katika kata ya Kifanya.

"Kata nzima ya Kifanya haina Mochwari na kama mnavyojua serikali ilipiga marufuku kulala na wapendwa wetu wanapotoweka duniani adha hii imesababisha wananchi kujiongeza mtu anapofariki na kusema mgonjwa amezidiwa kumbe ameshaaga dunia ili kuepuka gharama za kuutoa mwili kutoka Kifanya,kwa hiyo taarifa za mgonjwa kufariki wanaanza kueneza kesho yake asubuhi"alisema Kelvin Mwinuka mratibu wa mradi.

Shigela Ganja ni mchumi wa halmashauri ya mji wa Njombe,kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri katika mdahalo huo amekiri uwepo wa changamoto ya Mochwari katika kata ya Kifanya huku akibainisha kuwa halmashauri inajenga vituo vingi vya afya kwa mapato ya ndani hivyo wanaamini kushughulikia changamoto hiyo.

"Ni kweli ukienda pale wananchi wanataka mochwari yaani hata bila hayo majengo ya upasuaji na nini mkiuliza mnataka nini wanakwambia Mochwari lakini niwahakikishie tuna miradi,vituo karibu vitano vinatumia mapato ya ndani vyote hivyo tunaingiza fedha"alisema Ganja

Aidha katika maadhimio ya mdahalo huo baadhi ya wajumbe wakiwemo wenyeviti vijiji kutoka kata hiyo licha ya mapendekezo mengine wameomba kujengwa Mochwari katika kituo cha afya Kifanya ili kuondoa adha wanayokutana nayo wananchi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...