katika Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepata nafasi ya kutoa maada juu ya Mikakati ya Serikali katika kuliwezesha Jeshi pamoja na Wajibu wa Wakuu wa Wilaya katika kushirikiana na Jeshi hilo ili kukabiliana na Changamoto za Majanga.

Akiwasilisha maada hiyo kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Msemaji wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Anjela Kairuki, amewashukuru sana Wakuu wa Wilaya kwa namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ngazi za wilaya.

SACF Nzalayaimisi amesema ni wajibu wa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Jeshi hilo kuhakikisha kinga na tahadhari dhidi ya majanga mbalimbali huchukuliwa, ikiwa ni pamoja na usomaji na upitishwaji wa michoro ya ramani za majengo kabla majengo hayajajengwa  kupitia ofisi za Wakurugenzi pamoja na kutenga maeneo katika Wilaya zao kwa ajili ya ujenzi wa vituo na nyumba za makaazi kwa ajili ya Askari wa Zimamoto.

Aidha amewataka kujua kuwa Majanga mbalimbali hususani ya moto katika maeneo ya makaazi yamekuwa ni adui mkubwa katika kuleta maendeleo kwa jamii husika. Ni wajibu wa Viongozi wenye mamlaka ya kuongoza Mikoa na Wilaya zote kujikita zaidi katika tahadhari ya majanga hayo. Ni wajibu wa Viongozi hao kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kujikinga na namna ya kukabiliana na majanga hayo pale yanapotokea katika meneo yao.

Mafunzo hayo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara yanayomalizika leo, yalifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango Machi 13, 2023.

Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi akiwasilisha maada katika Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara katika Ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma leo tarehe 17 Machi, 2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...