Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua tawi jipya lililopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya huku wito ukitolewa kwa wafanyabiashara na wakazi wa mkoa huo kuchangamkia fursa za kiuwezeshaji kiuchumi zinazoletwa na benki hiyo mkoani humo.
Hafla ya uzinduzi wa tawi hilo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Bw Benno Malisa aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Bw Juma Homera na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi waandamizi wa benki hiyo na wafanyakazi, wawakilishi wa jumuiya ya wafanyabiashara pamoja na wananchi
Akizungumza kwa niaba ya RC Homera, Bw Malisa alisema mitaji ya fedha ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi hivyo uwepo benki ya NBC eneo hilo la Mwanjelwa utakuwa na tija zaidi iwapo tu wakazi wataitumia vema fursa hiyo.
“Najua fika kwamba kusogezewa karibu huduma za kifedha ikiwemo benki kama hivi ni jambo moja na kutumia ipasavyo uwepo wa huduma hizi ni jambo lingine. Ndio maana nawaomba sana wananchi wa Mwanjelwa kutumia vema fursa inayotolewa na benki ya NBC kutunza akiba zenu na pia kukopa ili kuwekeza na kukuza biashara zenu,’’ alisema.
Hata hivyo Bw Malisa alitoa rai kwa benki ya NBC kuendelea kubuni mipango mbalimbali ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia benki sambamba na kuongeza huduma zinazowagusa wananchi wenye hali ya kawaida kiuchumi ili waweze kukuza uchumi binafsi na kupanua uchumi kwa ujumla.
“Nafahamu Benki ya NBC mmekua mkibuni njia mbadala za kuwahudumia wateja kupitia njia mbalimbali ikiwemo kupitia mawakala na huduma kupitia simu yaani NBC Kiganjani, NBC Shambani na nyingine nyingi, Nawapongeza sana. Hata hivyo naomba sana endeleeni kuwaelimisha wateja wenu namna ya kutumia fursa za kibenki na kujiweza na kujikomboa kiuchumi.’’ Alisema
“Mkoa wa Mbeya kwa sasa unakuwa kwa kasi sana na wakazi wanaongezeka kila siku huku shughuli za kiuchumi pia zikiongezeka. Ongezeko hili la watu na ukuaji wa kiuchumi unahitaji kwenda sambamba na huduma mbalimbali ikiwemo hii ya kifedha…tunawashukuru sana na NBC kwa kuliona hili na kutusogezea huduma za kifedha Mwanjelwa,’’ aliongeza.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mkurugenzi Wateja Binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke alisema benki hiyo ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 30 inaendelea kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuwawezesha wajasiliamari na wakulima na wazalishaji wengine katika sekta za uchumi kwa kwa kutoa mitaji ya kifedha na mikopo nafuu.
“Jitihada hizi tunazitekeleza kwa urahisi zaidi kutokana wingi wamatawi yetu katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Tawi hili jipya la mwanjelwa tunalolifungua leo linafanya Benki ya NBC sasa kuwa na jumla ya matawi mawili hapa mkoani Mbeya na hivyo na kufanya jumla ya matawi yetu kufika 52 kote nchini.’’
“Kupitia matawi haya tumekuwa tukihudumia makundi yote ya jamii ikiwemo taasisi za serikali, watumishi wa serikali, wakulima, wafanyabiashara, wanafunzi sambamba na kukusanya maduhuli ya serikali kupitia Mfumo wa Ukusanyaji wa Fedha za Umma (GePG) na kodi kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).’’ Alitaja.
Kwa mujibu wa Bw Masuke uwepo wa tawi hili la Mwanjelwa ni matumaini ya kutatua changamoto iliyokuwepo kwa wateja wa benki hiyo Mkoani humo ambao waliokuwa wanalazimika kulifuata tawi mama lililopo Mbeya mjini ili kupata huduma.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Bw Benno Malisa ( alievaa suti nyeupe) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la benki ya NBC eneo la Mwanjelwa Mkoani Mbeya wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa tawi hilo iliyofanyika mkoani humo mapema hii leo. Wengine ni pamoja na Muwakilishi wa Mkurugenzi jiji la Mbeya Bw Gregory Emmanuel (wa tatu kulia), Mjumbe wa Bodi ya NBC Bw Godfrey Malekano (wa tano kushoto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa benki hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Bw Benno Malisa ( wa tatu kushoto) akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la benki ya NBC eneo la Mwanjelwa Mkoani Mbeya wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa tawi hilo iliyofanyika mkoani humo mapema hii leo. Wengine ni pamoja na Mjumbe wa Bodi ya NBC Bw Godfrey Malekano (wa tano kulia), Mkurugenzi Wateja Binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (wa tatu kulia), Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Dk Kassim Hussein ( Kulia) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa benki hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Bw Benno Malisa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Wateja Binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Muwakilishi wa Mkurugenzi jiji la Mbeya Bw Gregory Emmanuel akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Hafla hiyo iliambatana na burudani mbalimbali.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC pamoja na wateja wa benki hiyo wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Bw Benno Malisa (wa pili kushoto) Meneja wa Benki ya NBC tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (kushoto) akielezea kuhusiana na huduma za benki hiyo tawi jipya la Mwanjelwa Mkoani Mbeya wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa tawi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Bw Benno Malisa (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali, wateja pamoja na maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakati wa hafla hiyo.
Tujipongeze! Ndivyo wanavyoonekana kusema wafanyakazi wa benki ya NBC ikiwa ni ishara ya kujipongeza kwa kufanikisha uzinduzi wa tawi la benki hiyo eneo la Mwanjelwa Mkoani Mbeya.
Home
HABARI
NBC Yazindua Tawi Jipya Mwanjelwa Mbeya, Wananchi Waombwa Kuchangamkia Fursa za Kiuchumi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...