Kampuni ya Simu ya mkononi ya Airtel leo imeendelea na maonesho ya baadhi ya Huduma na bidhaa wanazotoa ambapo waheshimiwa wabunge na viongoz mbali mbali wamejitokeza kwa Lengo la kupata huduma zao.
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Dkt Tulia Akson aliingoza wabunge wengine leo kupata Huduma kutoka kwa wadau wa Mawasiliano ambapo pia alitembelea banda la Airtel viwanjani hapo.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alimkaribisha Spika na kumpatia ZAWADI Maalum ya Rauter ya Intanet inayoweza kuunganisha watu zaidi ya 32 kwa Wakati mmoja na Kisha kumweleza mheshimiwa Spika kuwa Airtel inamkabidhi zawadi kwa kuwa inajiamini sasa hata akiwa mkoani (Jimboni) ataunganishwa na Intaneti ye ye Kazi kwa kuwa asilimia 90 ya Minara ya Airtel sasa ya imeunganishwa teknolojia ya 4G ikiwemo Minara ya mbeya.
Maonesho ya wadau wa Mawasiliano yanaendelea kwa siku 3 katika viwanja vya bunge ikiwa ni kuelekea kwenye bunge la bajeti ya Mawasiliano linalotarajiwa kusomwa kesho na Waziri wa Habari na Mawasiliano Mheshimiwa Nape Mnauye.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt.Pindi Chana (MB) ni mmoja wa wageni waliotembelea banda la Airtel katika viwanja vya bunge na kuipongeza Airtel kwa mpango wake juu ya uwepo wa simu janja za mkopo kwenye maduka yote nchini. Airtel inaompango wa kutanua wigo wa matumizi wa simu janja (smartphone) kwa kuweka mpango bora wakukosha simu na kulipia kidogo kidogo kwa gharama ya hadi elfu 7 kwa wiki
Mbunge wa Mbulu Vijijini Mheshimiwa Fratery Massay akipata maelekezo toka kwa watoa Huduma wa Airtel Wakati wa maonesho ya wadau wa Mawasiliano katika viwanja vya bunge leo ambapo Airtel wamehudhuria wakingoja kusoma kwa bajeti ya Mawasiliano hapo kesho.
Mwandishi Mkongwe wa habari za picha bw, Deus Mhagale akipata maelezo kuhusu Vifaa vya home INTERNET vya Airtel Vinavyoweza kuunganisha hadi watu/vifaa 32 kwa Wakati mmoja kwenye viwanja vya bunge leo ambapo Airtel Wapo kwenye maonesho ya wadau wa Mawasiliano
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...