Na Jane Edward,Arusha .
Baadhi ya wazazi nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuwachagulia watoto fani ya kusomea kwani kwa kufanya hivyo kunashusha hari na ufanisi wa mtoto katika kujituma kwenye kazi pindi anapohitimu masomo yake.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko,chuo kikuu Mzumbe ,Rose Joseph katika maonyesho ya elimu ya ufundi yanayoendelea kufanyika jijini Arusha.
Amesema kuwa wapo wazazi ambao hawampi mtoto nafasi ya kumsikiliza anapenda kusomea fani gani na hivyo mtoto kujikuta akiingia kwenye masomo ambayo hayataki ambapo hali hiyo hudhoofisha ufaulu na ufanisi wa mtoto.
Rose anasema wao kama Mzumbe wanajitahidi kuhakikisha mtoto anapofika Chuoni hapo kwanza wajue anachokipenda ambapo hali hiyo huwalazimu kama chuo kumuhamisha mtoto na kumpeleka kwenye bunifu anayoifurahia yeye.
"Tushirikiane kwa pamoja wazazi kutambua matakwa ya mtoto na sio kuwa sehemu ya kutaka mtoto afanye wanachotaka wazazi hiyo imekuwa changamoto kubwa"amesema Rose
Akizungumzia shughuli wanazofanya kupitia Chuo kikuu cha Umma cha Mzumbe ambacho pia ni chuo cha utafiti ambapo amesema wanawezesha taasisi za elimu ya juu na ufundi stadi ambapo wanatoa elimu kuanzia cheti
Aidha anasema chuo hicho kimekuwa kikizalisha viongozi na watu mbalimbali kutokana na elimu wanayoitoa na wanajivunia kuwepo kwenye maonyesho hayo ya elimu kwa kuwa hakuna mahali utakapo pita usikutane na zao la Chuo cha Mzumbe.
"Sisi tunaweza kusema tunatembea kifua mbele kwakuwa tuna watu waliopita hapa Chuoni ikiwemo Rais wa sasa Dkt Samia suluhu Hassan ni zao la Chuo hiki,Spika mstaafu Anna Makinda pia ni zao letu kwahiyo tunajivunia kwakweli"Alisema Rose.


.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...