Tanzania imepokea habari njema kuhusu mradi wa umeme ambao utasaidia kuimarisha shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika mgodi wa STAMIGOLD, uliopo katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), mradi huu umekamilika na umegharimu takribani Bilioni 15.9.

Mradi huu wa umeme ulikamilika mnamo tarehe 20 Aprili 2023 na STAMIGOLD walianza kutumia umeme wa gridi ya Taifa tarehe 26 Aprili 2023. Njia ya umeme iliyojengwa ni ya ukubwa wa kilovolti 33 na imejengwa kwa umbali wa kilometa 105 kutoka kituo cha kupokea umeme cha Mpomvu - Geita. Ujenzi wa njia hii ya kusafirisha umeme pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha STAMIGOLD umefanikishwa kwa ushirikiano kati ya TANESCO na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha STAMIGOLD kimejengwa kwa transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 10 kila moja, na transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 2.5. Kwa ujumla, mradi huu unatarajiwa kuimarisha uzalishaji wa STAMIGOLD na kusaidia kuongeza mapato ya serikali kutokana na ushuru unaolipwa na kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, ACP. Advera Bulimba ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza Wilayani humo kutokana na uwepo wa umeme wa uhakika. Kwa kuwa STAMIGOLD ni miongoni mwa kampuni kubwa zinazochimba dhahabu nchini, ni matumaini ya serikali kuwa mradi huu utaongeza uzalishaji wa madini na kuimarisha uchumi wa taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...