MWANANCHI Thomas Nkola maarufu kwa jina la Mkulima amewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiomba kuwashtaki baadhi ya Mawaziri, Wakuu wa Taasisi na Kampuni binafsi yaliyohusishwa na ubadhirifu wa fedha za umma katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Sh.Trilioni 8.4

Mkulima amewasilisha mashauri matano mahakamani hapo ambayo yamefunguliwa leo Mei 11, 2023 na tayari yamesajiliwa na kupangiwa Mahakimu wa kuyasikiliza.

Akizungumza baada ya kusajiliwa kwa mashauri hayo, Wakili wa Thomas, Penina Ernest amedai kuwa maombi hayo matano yanahusu ubadhirifu wa fedha za umma zilizotokana na ripoti ya CAG 2021/2022.

Amedai mteja wake amefungua maombi hayo chini ya ibara ya 27 (1)(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inampa haki mwananchi yoyote kufungua kesi kama akiona kuna ubadhirifu wa fedha za umma, ili wanaohusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheri ikiwemo kufilisiwa ana kurudisha fedha umma.

Wakili Penina amewataja baadhi ya watu aliowafungulia maombi hayo ni Waziri wa fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, Japhet Justine, Mkurugenzi wa Mashitaka pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( TAKUKURU) ambao anadai wameisababishia Serikali hasara ya Sh.Trilioni 1. 285.

Wengine aliowataja ni Waziri wa Nishati January Makamba, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Maharage Chande na Habinder Seth ambao kwa mujibu wa Mkulima amedai wamesababisha hasara ya Sh.Bilioni 342.

Akizungumza nje ya Mahakama ameishukuru Mahakama kwa kukubali kufungua mombi hayo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...