Na Mwandishi wetu
AKIBA Commercial Bank Plc imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya fedha kwa vijana na umma kwa ujumla hususan katika nyanja ya kujiwekea Akiba, huduma za Mikopo, mpango wa fedha na kupanga bajeti za mtumizi binafsi na Biashara ili kusaidia kukuza uchimi wao.
Hayo yamesemwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda wakati alipotembelea tamasha la vijana linalojulikaba kwa "Kijana Janjaruka " ambapo Akiba Commercial Bank Plc ilishiriki kikamilifu lililoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambalo lilianza Mei 20-24 ,2023 katika viwanja vya Zakhem-Mbagala
Lengo la tamasha hilo ni kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana na maeneo ya jirani, kualika taasisi za fedha hususan mabenki ili kutoa elimu ya fedha kwa vijana na Akiba Bank kuonyesha bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na mabenki na taasisi nyingine.
Mkuu wa Wilaya Mwanahamisi alitembelea banda la Akiba Commercial Bank Plc katika viwanja hivyo siku ya tarehe 22 Mei, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kufahamu fursa mbalimbali zitolewazo kwa vijana kupitia Benki ya Akiba hususan huduma za Bima za BODASURE ambayo inalenga kutoa ulinzi kwa wamiliki na waendesha bodaboda na Bajaj.
Pia Mkuu Wilaya aliona fursa iliyozinduliwa na benki ya Akiba akaunti maalum kwa ajili ya Wanawake inayoitwa akaunti ya WARIDI ambayo ina masharti nafuu sana ya uendeshaji, lengo ni kuwainua Wanawake katika kufikia ndoto zao za mafanikio katika ujasiriamali.
"Mkuu wa Wilaya ya Temeke amefurahi na ameishukuru benki ya Akiba kwa kuonyesha mfano wa kuigwa kwa kutoa huduma bora jamii hivyo ameahidi kuendelea kushirikiana na taasisi za fedha hususan mabenki katika kuchochea maendeleo endelevu ndani ya Manispaa ya Temeke na Taifa kwa ujumla"amesema Mwanahamisi
Tamasha hilo lilifungwa Mei 24, 2023 huku likikadiriwa kukusanya zaidi ya vijana 200, 000 kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Temeke walionufaika kupata elimu ya fedha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...