Na Janeth Raphael - Michuzitv - Dodoma.


Mradi wa "USAID Kijana Nahodha umezinduliwa Tazania Bara, na ni mradi maalumu kwa vijana unaofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la maendeleo ya Kimataifa (USAID) uliopewa jina la " USAID Kijana Nahodha '

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dodoma Mkurugenzi wa mradi USAID Dkt Tuhuma Tulii amesema uzinduzi huo ni wa pili baada ya ule wa awali uliozinduliwa Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi mnano tarehe 23 mwezi wa pili mwaka huu 2023.

Dkt Tulii amesema mradi huo wa 'USAID kijana Nahodha' unatarajiwa kutekelezwa kwenye mikoa miwili ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es salaam na Morogoro pamoja na mikoa yote mitano ya Zanzibar.

" Utekelezaji wa mradi huu unaongozwa na T-MARC Tanzania kwa kushirikiana na mashirika ya Care International Tanzania Youth Coalition." amesema Dkt Tulii.

Mradi huo una dhamani ya dola milioni 1O.6 za kimarekani na unatarajiwa kuwawezesha vijana zaidi ya 45,000, vijana 15,000 kutoka Zanzibar na 30,000 kutoka mikoa ya Dar es salaam na Morogoro na mradi huo umewapa vipaumbele vijana wanaoishi na virusi vya UKIMWI, wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi na vijana wenye ulemavu.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa USAID Kate Somvong-siri amesema kuwashirikisha vijana kwenyew mipango mikakati ya maendeleo itawaweka katika nafasi nzuri ya kuunda na kutekeleza miradi itakayotatua changamoto kubwa zinazowakabili kwenye ulimwengu wa sasa.

"Kuwajengea uwezo vijana, kuwawekea miundombinu ya kupata huduma za afya na kuwaunganisha na fursa zilizopo kwenye Sekta muhimu za kiuchumi kama kilimo, utalii na uchumi wa buluu." amesema Kate Somvong-siri.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa USAID amesema vijana wa Kitanzania wataweza kujitegemea vyanzo vya mapato endelevu, kushiriki katika maswala ya kiuchumi na kuwa na raia wenye tija wanaochangia kikamilifi ukuaji wa uchumi wa nchi

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Patrobas Katambi amewahakikishia nchi washirika wa maendeleo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano katika kuwasaidia wananchi kiuchumi na hasa vijana.

Katambi amesema Serikali ya awamu ya sita imeanza kwenda maeneo ya TEHAMA kuhakikisha vijana wanaingia katika makundi mbalimbali ya biashara mtandao kupata elimu na ujuzi katika maeneo hay

"Tunapambana na kutokuadhirika kwa vijana na dawa za kulevya, UKIMWI na matumizi mabaya ya ukatili wa kijinsia na kuwafunza kuwa Watanzania wenye uzalendo na kuipenda nchi yao" Katambi.

NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Patrobas Katambi akipata maelezo kutoka kwa kijana aliyenufaika na mradi huo wa 'USAID KIJANA NAHODHA'
MKURUGENZI mkuu Mkazi wa USAID Kate Somvong-siri akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa 'USAID KIJANA NAHODHA'
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye ulemavu Patrobas Katambi akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa 'USAID KIJANA NAHODHA'
MKURUGENZI wa Mradi wa USAID Dkt Tuhuma Tulii akizungumza wakati wa uzinduzi wa 'USAID KIJANA NAHODHA ' jijini Dodoma.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...