Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja Wakubwa wa benki ya NBC Bw. James Meitaron (wa kwanza kulia ) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa ( wa Pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Bw. Elvis Ndunguru (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein wakati wa uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wkwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ).. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya. Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa akitoa hotuba kwa wageni waalikwa (hawapo pichani )wakati wa uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wakati wowote na mahali popote kwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ). Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Benki ya NBC mara baada ya uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wakati wowote na mahali popote kwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ). Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya[/caption] MBEYA Mei 1, 2023:
Benki ya Taifa ya Biashara ya (NBC) imezindua huduma ya NBC Connect, ikiwa ni ingizo jipya la huduma za kibunifu za kidijitali katika mkoa wa Mbeya. Huduma hiyo ya kisasa ya kidigitali inalenga kuwezesha huduma mbalimbali salama za kibenki na ambazo huweza kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa kutumia simu ya mkononi na vifaa vingine vinavyotumia Intaneti kwa mujibu wa Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa benki hiyo, Bw. James Metairon.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijiji Mbeya, Bw Metairon alibainisha kuwa kupitia NBC Connect, wateja wa mkoa huo na maeneo ya jirani watapata fursa ya kuwa na uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu mpya katika kupata huduma za kibenki.
“Huduma hii itawapa wateja wetu uwezo wa kufanya aina zote za malipo ikiwa ni pamoja na malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya Serikali pamoja na malipo kwa mitandao mbali mbali ya simu za mkononi kwa kutumia simu kompyuta, au simu zao za mkononi. Wateja pia wataweza kupata mwenendo wa miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki.’’ Alisema,
Kwa mujibu wa Bw Metairon, NBC Connect imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezibngatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo kuhakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.
"Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa Mbeya na maeneo ya jirani. Mfumo huu wa kibenki wa kidijitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama, na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja. NBC Connect itawawezesha wateja wetu kufanya huduma zakibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo." aliongeza Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, ujio wa huduma hiyo unatajwa kuwa utatoa usaidizi wa binafsi kwa wateja kupitia vituo vyao vya huduma kwa wateja ambapo kupitia mameneja katika vituo hivyo watawasaidia wateja kulingana na mahitaji yao na pia kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...