Na Mwandishi wetu

MUASISI Shule Huria ya Ukonga Skillfull, Diodorus Tabaro amewashauri wazazi na walezi kuwa licha ya kubanwa na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato cha kila siku, pia wanapaswa kuwa karibu na kusimamia malezi ya watoto wao.

Kauli hiyo imetoa wakati wa mahafali ya 15 ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule hiyo ambapo miongoni mwa wahitimu hao wapo waliofeli mtihani wa Taifa na kuamua kurudia na walioshindwa kuendelea na masomo miaka ya nyuma kutokana na sababu mbalimbali na kurudia kusoma kwa muda mfupi.

Amesema wazazi wengi wanashindwa kufanya majukumu yao ya malezi kwa kutokuwa karibu na watoto wao na kusababisha watoto wanaingia katika vitendo vya uvunjigu wa maadili.

“Wazazi wengi wamekuwa wakikimbizana na jukumu la kutafuta fedha jambo ambalo linasababisha walimu kuwa na wakati mgumu na kulazimika kuwa karibu na watoto kama walivyo wazazi,

"Ni muhimu wazazi kutumia muda mwingi kuwa karibu na watoto wao, mnapowapeleka shuleni zingatie kuwafuatilia kila hatua anayopitia hiyo itasaidia hata katika ufaulu wao, tumieni muda huo kuwaonyedha pia uhalisia wa maisha jinsi ulivyo, wasijaribu kuishi maisha ya mitandaoni yaani ‘fake life’ ambayo kwa sasa ndiyo yanawatesa vijana wengi nchini," amesema Tabaro.

Hata hivyo Tabaro amewataka wazazi na walezi kutowakatia tamaa vijana wao walioshindwa kupata alama nzuri za ufaulu katika mitihani ya kitaifa badala yake watafute njia za kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao.

Ameongeza katika shule hiyo ambayo inadahili wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na wale walioshindwa kuendelea na masomo na kushindwa kufanya mitihani ya taifa wamekuwa wakikutana na changamoto za wanafunzi waliokata tamaa ya kuendelea na masomo lakini walimu wa shule hiyo wamekuwa wakiwatia moyo ili waweze kufikia ndoto zao.

Amesema pamoja na changamoto hiyo shule yake imefanikiwa kuwabadilisha vijana wengi waliokuwa wamekata tamaa kwa kufeli katika mitihani ya kidato cha nne na wengine darasa la saba hadi kufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha sita.

Awali mwanafunzi anayemaliza kidato cha sita katika shule hiyo, Gilbert Binagi amesema vijana walioshindwa mitihani yao ya taifa wasikate tamaa kwani Ukonga Skillfull ipo kwa ajili ya kuweza kutumiza ndoto zao walizojiwekea.

Wakati huo huo Alphani Hamissi ambaye ni miongoni mwa wazazi wa watoto wanaosoma shule hiyo amesifu jitihada za walimu katika kuwafundisha wanafunzi waliopo kwenye shule hiyo kwani wanajitahidi kuhakikisha wanawafundisha vema na kuwa maendeleo mazuri yakielimu.

Muasisi wa Shule Huria ya Ukonga Skillfull, Diodorus Tabaro akiongea na wahitimu wa kidato Cha sita wa shule hiyo katika Mahafali ya 15 iliyofanyika jijini Dar  es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...