Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Mei 21, 2023 jijini Dar es Salaam amefungua wiki ya michezo kuelekea Siku ya Afrika Mei 25, 2023 iliyoandaliwa na Umoja wa Wanadiplomasia wa Afrika.

Akifungua michezo hiyo Mhe. Chana ameisisitiza Jamii kushiriki katika michezo na mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza pamoja na kulinda afya zao.

"Mhe. Rais Samia ameshatuelekeza kufanya mazoezi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, hivyo nasisitiza jambo hili kifanyika na kusimamia ipasavyo. Nawashukuru Wanadiplomasia Hawa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuandaa siku hii ya michezo hongereni sana" amesema.Mhe. Chana.

Bonanza hilo la michezo limeshirikisha timu za mpira wa miguu za watoto wa mabalozi, timu ya wake wa mabalozi na timu ya mabalozi dhidi ya timu ya Wizara ya Mambo ya Nje.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...