Na. Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa pongezi kwa Mtanzania Bi. Vick Elias kwa kuibuka wa kwanza katika mashindano ya Gofu ya Muthaiga Ladies Open 2023 yaliyomalizika hivi karibuni nchini Kenya.

Mhe. Chana ametoa pongezi hizo Mei 21, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifunga Mashindano ya Gofu ya Lugalo Ladies Open 2023, ambapo ametoa Rai kwa Wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki michezo mbalimbali hususani mchezo wa Gofu kwa kuwa katika dunia ya sasa michezo inatoa fursa ya ajira.

"Nalipongeza JWTZ na Klabu ya Gofu Lugalo kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi kutumia Klabu hii katika kuendeleza vipaji vyao na kukuza mchezo wa Gofu ambao unaendelea kukua siku hadi siku" amesema Mhe. Chana.

Awali Mwenyekiti wa Lugalo Gofu Club Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo amesema mashindano hayo yameshirikisha wanamichezo takriban 100 ambapo Wanawake ni zaidi ya 50.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...