Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametoa maagizo kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi iliyopo kwenye Kata ya Mboliboli, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ili ikamilike kwa wakati.

Kwa mujibu wa taarifa ya mradi wa skimu hiuo inayojengwa na Serikali kwa gharama ya Sh. Bilioni 58 na inatarajiwa kutumika kwenye mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 15,000 zilizopo eneo hilo ambalo linatumiwa na wakulima kuzalisha mpunga.

Akizungumza leo Mei 30, 2023 baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi huo , Chongolo amesema mradi huo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi 18 kama ambavyo mikataba ya wakandarasi wanaotekeleza imeainishwa.

"Tunataka wananchi waanze uzalishaji mapema na kuongeza tija ya kilimo katika eneo hilo.Naipongeza Serikali kwa kuanzisha mradi huu lakini ili tija yake ionekane Tume ya aTaifa ya Umwagiliaji inatakiwa kusimamia vizuri.

" Tutaweka msukumo ili fedha za kuwalipa wakandarasi zije kwa wakati,” amesema Katibu Mkuu huku akiwataka wakulima ambao wanaitumia skimu hiyo watunze miundombinu iliyopo ili itumike kwa muda mrefu na tija yake iendane na fedha ambazo serikali imezitoa kww ajili ya mradi huo.

Awali Ofisa Umwagiliaji wa Wilaya ya Iringa, Mhandisi Julius Lazaro ameeleza kwamba skimu hiyo ilianzishwa na wananchi walikuwa wanaitengeneza kwa kutumia mbinu za kienyeji na hivyo tija yake ilikuwa ndogo kwa sababu walikuwa wanazuia maji na mchanga.

"Wananchi walikuwa wanalima ekari 5,000 pekee kwa mwaka mzima lakini ujenzi wa mradi huu utakapokamilishwa watakuwa wanalima zaidi ya ekari 15,000 ambazo zipo kwenye bonde hilo."

Aidha amesema uzalishaji wa sasa ni tani 6,000 za mpunga lakini skimu hiyo itakapoanza kutumika wanatarajia kuzalisha tani 36,000, hivyo kuwainua wananchi wa eneo hilo kukua kiuchumi.

Kuhusu mkataba wa ujenzi wa skimu hiyo ni wa miezi 18 na ikikamilika itawasaidia wakulima kulima mara mbili kwa mwaka tofauti na ilivyosasa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo ya Mboliboli, Yusuph Samba ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali kwa kuiboresha skimu hiyo kwa maelezo kuwa walikuwa wanapata shida kwa muda mrefu na kulikuwa kunaibuka migogoro mingi.

Akizungumza kwenye mradi huo Katibu wa Halmashauri Kuu( NEC) Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewataka wananchi kutouza chakula chote baada ya kuvuna."Mkiuza chakula chote mnaweza kukUmbwa na baa la njaa na hivyo kusababisha uudumavu kwa watoto."


KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akizungumza leo Mei 30, 2023 baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi iliyopo kwenye Kata ya Mboliboli, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Chongolo amesema mradi huo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi 18 kama ambavyo mikataba ya wakandarasi wanaotekeleza imeainishwa na ametoa maagizo kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha wanasimamia mradi huo kikamilifu ili ukamilike kwa wakati.

Skimu hiyo inayojengwa na Serikali kwa gharama ya Sh. Bilioni 58 na inatarajiwa kutumika kwenye mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 15,000 zilizopo eneo hilo ambalo linatumiwa na wakulima kuzalisha mpunga. Katibu Mkuu ameambatana na wajumbe wawili wa sekretarieti ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema (wa tatu kulia) na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu (mwisho kushoto)


KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akizungumza na baadhi ya wataalamu wanaoendelea kujenga miundombinu ya mradi huo wa ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi iliyopo Kata ya Mboliboli, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa,kulia kwake ni Mbunge wa jimbo la Isimani Mhe.William Lukuvi
Ujenzi wa miundombinu ya mradi huo ikiendelea
Ofisa Umwagiliaji wa Wilaya ya Iringa, Mhandisi Julius Lazaro akitoa taarifa fupi kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (hayupo pichani) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi iliyopo Kata ya Mboliboli, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,mkoani Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...