

Njombe
JUMUIYA ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Njombe imesema kiasi cha shilingi Milioni 18,637,500 kimekusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali na kutumika kwenye ukarabati wa maduka ya jumuiya hiyo yaliyoteketea kwa moto April,1,2023 huku jumuiya ikihusika kuchangia Milioni 15,900,000.
Mwenyekiti wa Jumuiya wilaya ya Njombe Betreace Malekela amebainisha hayo wakati wakikabidhi milango kwa wafanyabiashara mara baada ya ukarabati ambapo amesema milango 9 ndio iliyokuwa imeteketea kabisa kwa moto huku wakiahidi kuongeza na kusogeza karibu miundombinu ya maji itakayosaidia kukabiliana na majanga ya moto.
"UWT wilaya ya Njombe tumechangia Milioni 15,900,000 wadau walituchangia shilingi Milioni 2,705,000 na jumla ya ghalama zote ni shilingi Milioni 18,637,500 wito wangu kwa wafanyabiashara tunaomba mdumishe upendo kati yenu na msiweke kisasi,tumefika hapa kwasababu ya visasi"amesema Betreace Malekela
Naye katibu wa UWT wilaya ya Njombe Sauda Mohamed amewaomba wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati pamoja na kuongeza usafi wa maeneo yao ya biashara hali ambayo itaongeza thamani ya biashara zao.
Baadhi ya wafanyabiashara akiwemo Aloyce Chaula na Elizabeth Mpogolo waliopatwa na changamoto hiyo ya moto kwenye maduka yao wamewashukuru wafanyabiashara wenzao kwa msaada walioutoa kwao wakati wa janga hilo huku pia wakiipongeza UWT kwa kukarabati milango kwa wakati na kuwakabidhi ili waendelee na biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...