Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV Mafinga.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Daniel Chongolo amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwamba barabara ambazo ziko kwenye mipango ya kuanza ujenzi yote itaanza ikiwemo barabara ya Igalambo A hadi Madibila.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mashujaa Mjini Mafinga Chongolo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa amezungumza na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa ambaye amesema ametenga bajeti ujenzi wa kilometa 10.
"Nimekutana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa , ameniambia fedha aliyonayo ni kilometa 10 , nimemwambia kilometa 10 hapana , tena sio kilometa 10 inayoanzia kule mbele , yaani watu wanatoka Igalambo A halafu wanakula vumbi kilometa 18 hapana , tumezungumza na Waziri Mbarawa tumekubaliana anaweka awamu ya kwanza kilometa 20 kutoka Igalambo A kwenda Madibila
" Na ataendelea kuongeza kila muda mkandarasi anapomaliza kipande cha kwanza lengo kilometa 58 ziishe , sasa niwaambie mtu anayejua kusimamia na kufuatilia wala haina haja ya kusema naomba subirini mkandarasi aje ,
"Hatuwezi kuwa tunaleta mkandarasi na kilometa 10 halafu zinaanzia huku, pale matumaini hakuna, yaani vumbi unaanza hapa hapa mwanzoni sio sawa.Pia nimewaambia kuhusu kile ambacho tumezungumza na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Barabara ya Mafinga kwenda Mgororo , niwaambie kwanza kibali kimechelewa lakini sasa lazima ianze kwasababu imebeba uchumi mkubwa wa wananchi...
" Ni wilaya muhimu kiungo cha wakulima , wazalishaji pamoja na Mji pamoja na maeneo mengine , mbao zinazotoka huko ni nyingi sana, chai inayotoka huko ni nyingi sana , huko ndiko tunakotoa karatasi zetu lakini huko kuna wananchi wanaolima mazao mbalimbali parachichi na mengine, "amesema Chongolo.
Ameongeza kwambA wao ni viongozi hakuna haja ya kupigiwa makofi , ni lazima waseme kwa uhakika na utekelezeji ufanyike ,hiyo ndio kazi ya kiongozi" Ukikuta kiongozi anapiga maneno, hana uhakika anachokisema achana naye , niwahakikishie muda sio mrefu mkandarasi atasaini mkabata wa kuanza ujenzi na mimi ninaenda kusimamia hatua kwa hatua.
"Lakini kuna barabara nyingine inaanzia Nyororo kwenda Mtuango , ndio ilikuwa barabara tunapanda basi mpaka ufike unakoenda unabaki unacheza wimbo mmoja Unatanga na njia.Nani anakumbuka basi la Mkombozi , ukipanda utadhani unaenda Dar es Salaam kumbe uko ndani ya Wilaya moja ya Mufindi.
" Mambo yamebadilika lakini na barabara hizi nazo zibadilike na yenyewe nimeambiwa inasuasua bado mkandarasi hayuko site , nimewaihidi hapa viongozi wa Mkoa hizi barabara nazichukua tunakwenda kusimamia kuhakikisha zinatangazwa haraka , wakandarasi wanaingia site na kuanza kujenga.
"Hatuwezi kurudi hapa tena na maneno, turudi hapa na kuonesha tulisema mkandarasi anaingia site na yuko, kiongozi sio kupiga maneno ambayo hayatekelezeki, na wahakikishia mtuamini."




.jpeg)




Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas akisalimiana na baadhi ya wananchi katika katika uwanja wa Mashujaa ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Godfrey Chongolo alifanya mkutano wa hadhara kwa kuzungumza na wananchi


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akishiriki ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Mwongozo inayojengwa chini ya mradi wa BOOST ambapo zaidi ya milioni mia tatu aroibaini na saba na laki tano (347,500,000/-) zimeshatolewa . Katibu Mkuu yupo kwenye ziara pamoja na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongoloakipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga dkt. Bonaventura Chitopela (kushoto) juu ya maendeleo ya mradi wa kituo cha afya Ifungo.
Katibu Mkuu yupo ziarani mkoani Iringa akiwa ameambatana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi Gavu na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...