Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mtendaji wa GS1 Tanzania na Mwenyekiti wa Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi Taifa, Fatma Kange, ametoa rai kwa wananchi na wafanyabiashara , kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho ya siku ya Barcode Tanzania.
Katika maadhimisho hayo yanayokwenda sambamba na manesho ambayo yatafunguliwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenyemahitaji maalumu, Dorothy Gwajima, yanatarajiwa kufanyika Juni 15-19, mwaka huu yakihusisha wafanyabiashara 400 na Mabanda zaidi ya 100.
Akifafanua zaidi mbele ya waandishi wa habari leo Mei 27, 2023 Kange amesema Barcode ni mistari ya namba inayowekwa kwenye bidhaa husika huku akieleza lengo la kuwepo kwa maadhimisho hayo ni pamoja na kuwasaidia wafanyabiashara kutambulisha biashara zao Kimataifa.
Aidha amewataka wafanyabiaahara wote kuzifanya biashara zao kuwa za viwango kwa kuweka Barcode huku akitaja faida moja wapo ya kufanya hivyo kuwa ni pamoja na kufanya kwa urahisi ukaguzi wa bidhaa zilizotoka na kutobadilika bei mara kwa mara.
Ametaja faida kwa upande wa mnunuzi kuwa ni pamoja na kwenda kirahisi sokoni, lakini pia kuitambulisha nchi husika Kimataifa.
"Katika maonesho hayo ambayo yatahudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwepo wajasiriamali,watumishi wa Serikali pamoja na wadau, kutakuwa na tuzo, ambayo itatolewa kwa taasisi ambayo imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa GS1 katika kutambua mchango wao katika maonesho hayo.
Home
BIASHARA
MKURUGENZI MTENDAJI GS1 TANZANIA AZUNGUMZIA MAADHIMISHO YA BARCODE YATAKAYOFANYIKA JUNI 15-19
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...