Na Pamela Mollel,Arusha

Katika jitihada za kuunga mkono serikali malengo ya kufikisha idadi ya watalii milioni 5 ifikapo 2025, maonyesho ya KARIBU-KILL FAIR yametajwa kuwa chachu ya kufikia malengo hayo.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kuanza juni mbili (2) hadi sita (6) yanalengo la kukutanisha wadau wa utalii kutoka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa TATO Hendry Kimambo amesema maonyesho hayo ni fursa kwa wafanyabiashara ya utalii kujiuza lakini pia kujua bidhaa mpya za utalii zilizopo sokoni ili kuwavutia watalii wengi zaidi Tanzania.

Kwa upande wake Dominic Shoo ambaye ni mmoja wa waandaaji wa maonyesho hayo amesema onyesho hilo limekuwa ni sehemu ya kuwaleta wageni kuona uzuri wa Tanzania ambapo kila mwaka linaleta wageni zaidi ya 500 kutoka nje ya nchi.

"Tangu tumeanza maonyesho wageni wamekuwa wakiongezeka kila mwaka hivyo kwa nchi yetu tumekuwa sehemu ya kuchangia pato la taifa" amesema Shoo.

Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa bank ya CRDB Boma Rabilla ambaye alikabidhi hundi ya milioni 50 ikiwa ni sehemu ya mchango wa kufanikisha maonyesho hayo amesema kuna haja ya kuunga mkono jitihada zozote za kuongeza watalii.

"Ikitoka biashara ya dhahabu iliyoingiza Bilioni 2.8 za kimarekani inayofuata ni sekta ya utalii iliyoingiza Bilioni 2.4 hivyo kufanikisha maonyesho haya ni kufanikisha kuongeza fedha za kigeni nchini" amesema Rabilla.

Maonyesho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya magereza yatashirikisha wageni kutoka nchi mbalimbali na mataifa yameendelea kuthibitisha ushiriki.

Afisa mtendaji mkuu wa benki ya CRDB Boma Rabilla alikabidhi hundi ya milioni 50 waandaaji wa maonyesho ya KARIBU KILL FAIR, Dominic Shoo wakwanza kulia na Tom Kunkler wapili kutoka kulia

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...