Na. Damian Kunambi

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema tayari amekwisha wapata watu watatu kati ya sita ambao walifadhiliwa na Mwl. Julius Kambarage Nyerere kupata mafunzo nje ya nchi juu ya Liganga na Mchuchuma ambapo waliweza kubaini aina mbalimbali madini zilizopo katika miradi hiyo.

Akizungumza hayo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao mbunge huyo amesema kipindi hicho hakukuwa na utalaam wa namna ya kutenganisha madini hayo yaliyouganika lakini kwa sasa teknolojia imekua na kuwa na uwezo wa kutenganisha hivyo anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini uanzishwaji wa miradi hiyo na kutoa fedha kiasi cha Sh. Bl. 15.5 ili kuwalipa wananchi wanaopisha miradi hiyo.

" Nimshukuru sana Rais wetu wa Tanzania kwa kufanikisha juhudi ambazo zilizianzishwa na watangulizi wake kwani kwa sasa historia ya Ludewa inaenda kubadilika kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla".

Sanjari na hilo pia mbunge huyo aliwataka wananchi hao kutumia fedha za fidia wanazotarajiwa kulipwa hivi karibuni kwani endapo hawatazitumia kwa malengo ya kuzizalisha wanaweza ona kama miradi hiyo haikuwanufaisha chochote.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilayani Ludewa Stanley Kolimba ambaye pia aliwahi kuwa mbunge kwa kipindi cha mwaka 2000 hadi 2005 amesema wabunge wengi wamepita katika jimbo hilo akiwemo yeye ambapo wamekuwa wakipiga kelele bungeni juu ya ulipaji fidia hizo sambamba na kuanzishwa kwa miradi hiyo lakini hakukuwa na matokeo yoyote.

"Mfupa uliotushinda sisi watangulizi umewezwa na mbunge wa sasa ambaye ni Kamonga, binafsi nimpongeze Kamonga pamoja na Rais wetu kwa kufanikisha hili kwani kilio hiki kilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi hawa"

Fidia hiyo ambayo ilisubiliwa kwa miaka mingi inaenda kunufaisha wananchi 650 katika kata ya Nkomang'ombe ambapo serikali imekwisha toa kiasi cha sh. Bl. 5.2 kwaajili ya malipo ya wananchi hao.

Nae muwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Florian Mramba amesema kwa sasa tayari wametangasa tenda ya kupata makampuni makubwa matano ambao wanatakiwa kuwa na mitaji isiyopungua kiasi cha Sh. Bl. 5.

Amesema makampuni hayo yataanza uchimbaji huo wa madini ya makaa ya mawe mara baada ya kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi hao ambao wanatarajia kulipwa siku chache zijazo.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...