*Atoa maelekezo kwa mizigo iliyoko stoo, ampa maagizo Kamishina TRA

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

BAADA ya wafanyabiashara wa Kariakoo na maeneo mengine nchini kulalamikia utaratibu unaotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) katika kukusanya kodi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametanza rasmi kuiondoa Task Force iliyokuwa imeundwa na mamlaka hiyo kwa ajili ya kukusanya kodi.

Kitendo cha Waziri Mkuu kutoa maagizo ya kuondoa Task force hiyo wafanyabiashara waliokuwa kwenye kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu kwa maelekezo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan shangwe ziliibuka kwa wafanyabishara kwani kitengo cha task force wamedai kimekuwa kero kubwa kwao.

Akitangaza uamuzi huo kwenye kikao hicho cha wafanyabiara na Waziri Mkuu kilichochukua saa tano, Waziri Mkuu Majaliwa amesema anaivunja Task force na kwamba kuanzia sasa hakuna task force kwani imeleta watu ambao hawajasomea mambo ya kodi.

“Hii Task foce ya imeleta vijana wenye kozi mpya ambao wameingia humo wamekuja na shida zao na tamaa tama za maisha hapana. Kodi itakusanywa na maofisa wetu wa TRA ambao wamesomea na maadili ili wakikosea tutawabana kwa maadili yao.

“Lakini pia tumesikia hapa watoza kodi wengine Jeshi la Polisi, najua jukumu la Polisi ni kulinda mali na watu kazi ya kukagua risiti sio wao mpaka tu pale watakapokuwa wamekuja kwa dhamana hiyo na wakajitambulisha kama sisi ni wakaguzi tumekuja kukukagua na wakaonesha na kibali.

“Hilo ndilo jukumu la Jeshi la Polisi na kazi hiyo itaendelea, lakini kwenda Kariakoo kukusanya kodi italeta mkanganyiko, lawama zinakuwa nyingi kwa taasisi yetu, zinakuwa nyingi serikalini lakini sisi watendaji tuliopewa dhamana na Rais haturuhusu hali hii ikaendelea.Kwa hiyo hii task force hii tunaiondoa

Kuhusu tozo za stoo , ameambia wafanyabiashara iko sheria yamaghala inayotekelezwa na Wizara ya Viwanda na Biashara haina mgogoro, kila mwenye stoo kwa kuwa anafanyabiashara kwa kitendo cha kufanyabiashara analipa kodi na ni kitendo cha kawaida.

“Kama kuna stoo nyingine analipwa kodi, najua biashara mnazofanya jioni hamrudi nazo kuna mahali mnapeleka huyo mnamlipa na yeye anatakiwa kulipa , huyo huyo sio nyie, kama stoo inayotozwa tozo na wizara ya viwanda na biashara haina kero kwanini kero zije kwenye wafanyabiashara?

“Kuna dosari hapa nipo na Mkurugenzi wa stakabadhi ghalani yeye ndio mwenye sheria ile na anatoza tozo kwenye maghala haina kelele na wanalipa kwenye viwanda, kwanini kelele ziibuke TRA?Maana yake sheria hiyo iliyopo sio mbaya lakini kuna kanuni hapa ambazo huenda zimetengeza mianya ya kuleta kero.

“Kwa hiyo kanuni hizo nazisitisha mpaka hapo zitakapoangaliwa upya na tangu juzi nilipotamka lilishasimama, watangaalia kwanini ina mgogoro , wataangalia kama inamleta hasara mfanyabishara na kama mfanyabiashara wenyewe ni nyie mnachukua biashara kwenda kuweka stoo ni ya mwenye stoo , nyie mnapeleka kwa makubaliano yenu.

“Lakini mwenye stoo kwa kuwa anapata mapato lazima alipe kodi lakini shida ilikuwa ni pale ilipokuwa inahusisha tozo za mzigo halafu inakuja kuunganishwa na tozo ya stoo ikaleta maana mbovu.”amesema Waziri Mkuu alipokuwa akijibu hoja moja baada ya nyingine za wafanyabiashara hao.

Kuhusu mizigo iliyokamatwa ,Waziri Mkuu amesema wameaambiwa ziko stoo ambazo zimerundika mizigo ya wafanyabiashara na mingine mpaka inafikia hatua inaoza kwani aliyeweka anaogopa kwenda kuchukua maana akitaka kwenda anaambiwa kuna mtu anakamata.

“Sasa mizigo hii wale wote wenye mizigo mtoe taarifa kwa kamati hii.Tukisema itoke mara moja itakuwa tafaran, hivyo iratibiwe wale wenye mizigo Mtaa wa Kipata kamati chagua mtu mmoja akae huko halafu kila mmoja ataje mzigo wake.Kama tatizo lilikuwa ni kodi kamati mtaangalia nini cha kufanya, Kamishina wa TRA anasheria inamruhusu kurekebisha kodi.

“Mizigo imekaa sana mingine imepoteza thamani na mingine inataka kuoza , Kamishina uking’ang’ania ile hutapa chochote , nenda kaangalie utaratibu mwingine wa bei ndogo nafuu ili watu waweze kutoa, au achia kabisa, kamati itashauri.”


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...