*Awatolea uvuvi kudharau kauli za viongozi, asema iwe mwisho

*Awaangukia wafanyabiashara , awataka kurejesha wateja waliokimbia


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewaambia Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wasirudie tana kuwambia wafanyabishara wapeleke barua ya Rais kama ambavyo wamekuwa wakiwaambia licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa maelekezo kwa vyombo vinavyokusanya kodi kusamehe kodi ya miaka mitano nyuma kwa wafanyabiashara.

Miongoni mwa malalamiko ya wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaa na maeneo mengine ni kauli za baadhi ya watumishi wa TRA ambao walikuwa wanalazimisha wafanyabashara kuonesha barua ya Rais inayotaka kuwa amesamehe kodi jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa.

Akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo sambamba na wafanyabiara wa mikoani walioshiriki kikao hicho kilichofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam , Waziri Mkuu amesema ni kosa kubwa kudharau maelekezo ya viongozi.

“Kudharau kauli za viongozi narudia tena Waziri mwenye dhamana kwa wizara yake, Waziri Mkuu, Makamu wa rais na kigogo mwenyewe Rais hawa wakisema kuziambia mamlaka zao za chini ni agizo.Mnataka waandike barua wataandika barua ngapi?

“Waziri ataandika barua ngapi kuwaambia watu wake wa wizara likubwa lote hilo, Waziri Mkuu ataandika barua ngapi kwa Wizara zote na watendaji wote nchini. Rais ana ashughuli nyingi za kimataifa, Mamlaka ya Mapato tusisikie tena mkiomba barua kwa wafanyabiashara.

“Barua ya Rais eti wewe ndio ufanye kazi yako, kwani anapozungumza hamkai kwenye luninga, hamkai kwenye redio ? Ngoja nirudie niwape siri, ninapofanya ziara huwa nawakumbusha watumishi wa Serikali kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Makamu wa Rais , Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,Rais wa Zanzibar anapokuwa anazungumza kulihutubia taifa jipange kaa kwenye luninga muone.

“Chukua redio usikilize, na kila ataagiza na kitakugugusa kwenye eneo lako ni agizo, kwa hiyo ukiona unaguswa chukua kalamu weka kumbukumbu kwamba hili ni agizo langu. Nawakumbusha tena watumishi wenzangu wa Serikali viongozi wetu wanapokuwa wanahutubia taifa…

“Wanapozungumza na kundi kubwa la watu, anapozungumzia jambo maalum, chochote anachozungumza mtumishi kikigusa kwa kuagiza mtumishi nenda kashughulike mara moja usisubiri barua, nyine mkisikia mtu anasema barua ya Rais tutajieni jina tushughulike naye,”amesema Waziri Mkuu.

Amesisitiza anaamini hilo halitajirudia tena ,Kamishna wa TRA yuko na ataenda kuwaambia watendaji wake mpaka mikoani.

“Rais anatamka mnakuwa na mashaka , Rais wa nchi!! wee weee. Kama kuna haja ya kutumia njia ziko ndani ya serikali .Pamoja na hayo wafanyabiashara naomba muone nia ya dhati ya Serikali yenu inapenda mfanye biashara yenu na mpate mafanikio.

“Na Serikali yetu kupitia Rais wetu inawapenda mno na hii ndio dhamira tuliyokusudia , tunajua mna mikopo na mingine mikopo umiza ambayo inatarajia kufanyabiashara za siku wakalipe lakii maisha ya kila siku yanategemea mapato haya. 

Hatujaishia hapo tunajua mnahitaji kupanua biashara, tukipunguza siku moja inapunguza tija ya kufanyabiashara , siku hizi nne ambazo zimepotea nawaomba sana wafanyabiashara wete wa Tanzania hasa hili soko la kimataifa mjue soko hili ni soko la kimataifa

“Tumeshafungua milango kwa soko la Msumbiji, Malawi, Congo, Rwanda, Burundi , Kenya na Uganda wale waliondoka kwenda huko tuwarudishe , haipendezi kusikia nyie mnachukua shuka hapa kwa kuchukua Uganda wakati bandari inapita hapa.

“Haipendezi vitende vishuke hapa viende Zambia halafu virudi nyuma nyuma, haiwezekani, hatuna shida yoyote ile kama kuna sheria na kwenye maagizo yangu nitaiweka ili kuwe na unafuu , watanzania wanategemea maendeleo kwa kodi , kwa siku mbili hizi athari tumeipata lakini hatuwezi kulalamika kwani tunajua mlikuwa mnatumia njia hiyo kama mbinu ya kuonesha matatizo mliyonayo.

“Na mlifanya jitihada za kukutana na TRA, Wilaya na Mikoa mkaona bado,mkatumia mbinu hii na mmeona nimekuja, nataka niwahakikishie kuanzia leo mkipata matatizo wizara iko wazi nendeni , ofisi ya uratibu ya Waziri Mkuu iko wazi tutawasikiliza, hakuna jambo lolote.”


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...