Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kerege Kasika M. Kasika akiwakaribisha wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa elimu na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu pamoja na kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Kerege iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kerege iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kerege wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo Bagamoyo mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...