
Kaimu Afisa Mfawidhi TASAC Mkoa wa Mtwara Joseph Myaka akitoa elimu kwa Wavuvi wa Nyamisati juu ya umuhimu wa vifaa Uokozi wakati uvuaji kwa ajili ya Usalama wao na mali zao.
Matukio katika picha wakati wa TASAC wakitoa elumu ya Usalama Majini kwa Wavuvi Nyamisati Kibiti mkoani Pwani.
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu ya Usafiri Salama Majini kwa wadau mbalimbali wa Wilaya ya Kibiti katika mialo ya Nyamisati Mkoani Pwani tarehe 25 Mei, 2023.
Elimu hiyo iliyotolewa katika mialo iliyozunguka Nyamasati iliwajumuisha wavuvi, manahodha wa vyombo, wamiliki wa vyombo, wafanyabiashara na watumiaji wa vyombo vidogo vya usafiri majini.
Watoa mada mbalimbali kutoka TASAC, TPA na BMU walitoa elimu ya jinsi ya kutumia vifaa vya uokoaji pindi inapotokea dharura au ajali majini; utumiaji vifaa vya uokoaji pamoja na matumizi ya kizimia moto (fire extinguisher) na umuhimu wa kuwa na kifaa hicho kwenye vyombo vidogo vya majini.
TASAC imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri majini kutoa elimu katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuwahamasisha wamiliki wa vyombo kuweka vifaa vya kujiokolea lakini pia manahodha na wavuvi kuvaa jaketi okozi wakati wote wawapo safarini au kuendesha shughuli za uvuvi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...