Na Karama Kenyunko
WAKAZI watatu wa Morogoro Wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Wakikabiliwa na shtaka moja la unyanganyi wa kutumia silaha na kuiba simu.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Mei 29,2023 na wakili wa serikali Grace Mwanga imewataja washtakiwa hao kuwa ni Sufiani Kideku (30) na Celestine Kamuli (32) wote wanaishi Kizuka Morogoro na Hussein Mwinyijuma (41) Mkazi wa Gairo mkoani humo.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Feldnand Kihwonde imedaiwa kuwa, Mei 17, 2023 huko katika eneo la Zaramo mtaa wa Jamuhuri ndani ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam washtakiwa waliiba simu moja aina ya iPhone mali ya Hussein Mohamed.
Imeendelea kudaiwa kuwa washtakiwa mara baada ya wizi huo walimtishia Hussein kwa Pistol aina ya Luger na kisha kumteka Ili waweze kujipatia fedha.
Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kuwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha hayana dhamana.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 12,2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...