Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WAKATI Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 yakitarajia kuanza Juni 28 mwaka huu, Mkurugenzi wa Kampuni inayozalisha bidhaa zitokanazo na karanga ya Seasoning Palet Tobiproduct, Agatha Laizer ameeleza namna ambavyo amejipanga vema kwa kupeleka bidhaa zake kwenye maonesho hayo.
Ametumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo maonesho hayo ambayo yamekuwa yakifanyika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambavyo yamekuwa yakitoa fursa kwake na wafanyabiashara wengine wanavyoweza kutangaza biadhaa zao na kuonesha ubunifu wao katika kuzalisha bidhaa zinazokubalika soko la kitaifa na kimataifa.
Akizungumza leo Mei 19, 2023 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Maonyesho ya sabasaba vya Mwalimu Julius Nyerere Agatha Laizer amesema
kwa mwaka huu kampuni yake inatarajia kushiriki maonesho hayo kama ambavyo wamekuwa wakishiriki miaka yote na kubwa zaidi amewaomba wananchi pindi maonesho yayakaopoanza kufika kwenye banda lake kununua bidhaa zao.
Aidha amewatia moyo wafanyabiashara wenzake hasa wale wenye biashara ndogo ndogo katika maonyesho ya mwaka huu ya sabasaba wayatumie vizuri kujitangaza lakini kuongeza mtandao wa wateja pamoja na wafanyabiashara wengine.
"Tutakaposhiriki mwaka huu katika maonesho haya tutakuwa na uwezo wa kufanyakazi zaidi na kutengeneza mtandao mkubwa wa biashara ili kupata fursa ambazo zitakazotufanya tuzidi kuendelea mbele zaidi .Tunafahamu umuhimu wa maonesho haya na ndio maana tumeendelea kushiriki."
Agatha ametumia nafasi hiyo kuishukuru TanTrade kwa kuanza maandalizi ya maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu nmapema, hivyo amewataka wafanyabiashara hasa wanawake na vijana washiriki kikamilifu na wala hawana sababu za kubaki nyuma.
Amesema anatambua kuwa wafanyabiashara wa Tanzania wanazo biadhaa nzuri na zenye ubora ambazo zinaweza kushindana kwenye soko.
Pamoja na hayo ameendelea kuipongeza TanTrade kwa kuwashirikisha wafanyabiashara kwenye maandalizi kwaniaba ya wajasiriamali wengine, hivyo ni imani yake wafanyabiashara na wajasiriamali wengi watapata fursa ya kushiriki kikamilifu kwenye maonyesho hayo.
"Mimi kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Palet Tobi product tumejipanga vizuri kuwaletea bidhaa bora kwenye maonyesho ya kimaitafa ya sabasaba ambapo kwamujibu wa TanTrade kutakuwa washiriki wengi zaidi kutoka nje ya nchi na ndani ya Tanzania."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...