Na Jane Edward, Arusha

Wanawake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusomea kozi za uongozaji wa meli ili waweze kunufaika na fursa zote na kuweza kupata ajira kwa urahisi.

Akizungumza jijini Arusha Mhadhiri Msaidizi wa chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI),Azan Juma Azan katika Maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanayofanyika jijini Arusha.

Azan amesema kuwa, uwiano uliopo chuoni hapo kati ya wanawake na wanaume bado idadi ya wanawake ni ndogo ikilinganishwa na wanaume na hiyo ni kutokana na dhana iliyokuwepo ya kuwa kozi hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu.

Amesema kuwa wamefungua dirisha la usajili kwa ngazi ya cheti hadi diploma kwa dirisha la masomo Septemba hivyo wanatoa rai kwa watu mbalimbali kujitokeze kwa wingi .

Naye Mmoja wa wanafunzi ,Wilfrida Ngallu mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika shahada ya uhandisi wa meli na vifaa vya madini,amesema kuwa,pamoja na kuwa watu wanachukulia kozi hiyo kama kozi ya wanaume peke yake lakini yeye amedhubutu kusomea kwani ana shauku kubwa ya kusafiri duniani .
Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya UONGOZAJI MELI Eric Seaser kutoka chuo cha bahai dar es salam akitoa elimu ya matumizi ya vifaa vinavyohifadhiwa kwenye liferaft(kifaa cha uokoaji) kinachotumika kujiokolea wakati meli impepata dharura baharini.

Azan Mohamed Azan , Mhadhiri msaidizi kutoka chuo cha Bahari Dar es salaam akionesha namna ya kuvaa life jacket (kifaa cha kuokolea Maisha kwa wanafunzi wa shule ya sekondari kaloleni walipotembelea banda la DMI.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...