Njombe
JUMUIYA ya Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Njombe imetoa pongezi kwa madiwani wote wa viti maalumu kwa kufanikiwa kutembelea matawi 207 kuangalia hali halisi ya siasa pamoja na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Betreace Malekela ametoa pongezi hizo mara baada ya madiwani kufanya kazi kubwa ya kutekeleza zoezi hilo.

"Wakati tukifuatilia mwenendo wa ziara hizo tumewaona madiwani wakipambana kila mmoja na eneo lake na wakati wakipita wamekutana na wanawake wengi wakiangalia hali ya siasa,usajili wa wanachama lakini jambo jingine ni kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia"amesema Betreace

Ameongeza kuwa miongoni mwa jambo lililowapa faraja Jumuiya ni kuona namna madiwani hao walivyowatumia wataalamu kutoa elimu ikiwemo wataalamu wa uchumi kutoka kwenye mabenk kutoa elimu ya uchumi.

Ametoa wito kwa madiwani kuendelea kuzungumzia kazi nzuri zinazofanywa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kutokana na miradi mikubwa ambayo anaendelea kuitekeleza kwenye maeneo mbalimbali nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...