MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akizungumza katika ufunguzi wa warsha kwa wafanyakazi wa taasisi za kifedha kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa katika kampuni iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyeyere jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Usajili Kampuni na Majina ya Biashara, BRELA, Isdor Mkindi akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa warsha kwa wafanyakazi wa taasisi za kifedha kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa katika kampuni iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyeyere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Benki Tanzania, Tusekelege Joune akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa warsha kwa wafanyakazi wa taasisi za kifedha kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa katika kampuni iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyeyere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andrew Mkapa akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa warsha kwa wafanyakazi wa taasisi za kifedha kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa katika kampuni iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyeyere jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wahiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na BRELA.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewaomba wafanyakazi wa Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Taasisi za Kifedha kuweza kuwafichua wamiliki wa kampuni ambao hawajatoa taarifa zao na hawafahamiki ili waweze kufahamika.

Ameyasema hayo leo Juni 27,2023 wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila katika ufunguzi wa warsha kwa wafanyakazi wa taasisi za kifedha kuhusu utekelezaji wa kanuni za wamiliki manufaa katika kampuni iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyeyere jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa BRELA imekuwa ikishirikiana na taasisi za benki nchini katika shughuli mbalimbali hasa zinazohusu utendaji wa kampuni na majina ya biashara pamoja na kupeana taarifa za marekebisho na maboresho yanayoendelea kisheria na kimifumo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma sahihi na kwawakati.

"Yapo makampuni ambayo tayari yamepata mwitikio wa kutoa taarifa zao za kampuni na wamiliki wake.... Lakini yapo Makampuni mengi ambayo yamewekwa kwenye Blifcase hatujaenda kuyatolea taarifa zake lakini nani ataenda kutusaidia kuhakikisha makapuni yamesajiliwa...

Amesema jitihada za BRELA za kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali haziwezi kufanikiwa bila Taasisi za Kifedha ambao ni mhimu na kiungo kati ya sheria na maelekezo mbalimbali ya serikali.

Amesema kuwa taasisi za kifedha zishirikiane na mamlaka zilizopo ili kufanikisha lengo la sheria ya fedha ya mwaka 2020 na marekebisho ya sheria ya makampuni sura ya 212 na kuwezesha taarifa za wamiliki Manufaa katika kampuni.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Usajili Kampuni na Majina ya Biashara, BRELA, Isdor Mkindi amesema kuwa Mafunzo haya ambayo wanayatoa leo kwa Wafanyakazi wa Taasisi za kifedha ni mahusisi kwao kwani ndio wenye taarifa za watu mbalimbali kupitia akaunti zao za benki na makapuni mbalimbali.

Amesema Taasisi za Kifedha zinanafasi ya kutoa taarifa kwa sababu anahusika hasa kuhifadhi taarifa za watu na za kampuni ambapo mwisho wa siku kampuni hizo zinaweza kufanya uhalifu wa kifedha kwa kupitia benki.

Amesema wataalamu hao wa benki lazima wapate mbinu ambazo BRELA wanazo kwaajili ya kuweza kuwatambua na kutambua kampuni pamoja na kuweza kutoa taarifa zao kwenye vyombo vya uchunguzi.

Amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja mahususi ili kudhibiti makosa ya kifedha ulimwenguni ikiwa ni pamoja na kupunguza au kuondoa matatizo hayo.

"Mtu akiwasilisha taarifa za uongo au zisizo sahihi au kutoziwasilisha kabisa sheria imetoa kifungo jela na faini ya fedha zisizozidi milioni 10 kwa kosa hilo." Amesema

Akizungumzia manufaa ya sheria ya fedha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Benki Tanzania, Tusekelege Joune amesema kuwa sheria ya mwaka 2020 itaondoa watu wasio wamiliki wa kampuni kwa niaba ya tu mwingine ambao hawataki kujulikana au hawezi kuendesha biashara vizuri zaidi kuliko Mkurugenzi ambaye atakuwa sio mmiliki wa kampuni.

Amesema kuwa Mafunzo yanayotolewa na BRELA kwao ni mhimu kwasababu ni sheria iliyowekwa kwaajili ya kuongoza kisheria na sheria inatakiwa ifuatwe.

"Tumekuwa mstari wa mbele na nijukumu letu kuweza kutoa taarifa zozote ambazo zinamashaka au ni tofauti na matendo ya mtumiaji wa akaunti ya benki."

Akitolea mfano Tusekelage amesema benki inajukumu la kutoa taarifa za mmiliki wa akaunti ya benki itakayowekwa pesa nyingi kuliko kawaida ya kiasi ambacho huwa anakiweka mara nyingi huku kukiwa na shaka kuwa kiasi cha pesa hicho amekitoa wapi.

"Kwahiyo Sheria ambayo BRELA wanaisimamia, inatusimamia sasa kuweza kumjua mmiliki halali wa hiyo kampuni kwamba sio huyu tunayemwona kwenye makaratasi lakini anayetoa maamuzi ya mwisho au anayepata fungu kubwa kwenye kampuni hii ni nani, pia inatusaidia kukotro mambo ya uharifu wa kifedha, utakatishaji wa fedha kwa sababu watu ambao hawataki wajulikane kwani wanakuwa na nia ovu ambazo hawataki zijulikane kwamba hizi pesa zinatoka kwa nani, na kwanini hataki tumjue." Amesema

Aidha amesema kuwa mafunzo wanayoyapata yatawasaidia kuwa na uelewa wa pamoja na hawategemei kwenda kinyume na sheria.

Amesema kuwa mafunzo hayo kwa wafanyakazi wa taasisi za benki yatoa mwanga kuwa ni nani anatakiwa kutoa hizo taarifa na hata kama mtu anayetoa ushauri na unafanyiwa kazi lazima taarifa zake ziende BRELA.

Ikumbukwe kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Muswada wa sheria ya fedha 2020 lilipitisha marekebisho ya sheria ya Kampuni, Sura 212 kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa taarifa za 2amiliki manufaa katika kampuni ambazo ni muhimu katika kuboresha mazingira ya uwekezaji, kikodi pamoja na kudhibiti utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili wa vitendo vya ugaidi.

Aidha mwaka 2021 waziri mwenye dhamana alipotisha kanuni za umiliki manufaa katika kampuni ambazo zilipitishwa na kuanzaa kutumia rasmi mwaka 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...