Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Bahi
KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa( NEC) Oganaizesheni wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Issa Haji Gavu amesema Chama hicho hakitakuwa tayari kuwavumilia wenyeviti wa Vitongoji na vijiji ambao hawaitishi vikao vya kuelezea uwazi wa mapato na matumizi kwa wananchi wa maeneo husika.
Akizungumza leo akiwa Tawi la Shina Namba 18 katika Kata ya Bahi mkoani Dodoma ikiwa ni muendelezo wa ziara za Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Daniel Chongolo, Gavu ambaye yuko kwenye ziara hiyo amesema lazima viongozi hao wakajenga utamaduni wa kuitisha vikao vyenye ajenda za wananchi.
"Msipofanya vikao vya kuelezea mapato na matumizi, wenye viti wa vitongoji na vijiji maana yake wanatutengenezea ugumu katika ushindi wetu wa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024.
" Sisi kama CCM hatuko tayari kuvumilia kiongozi yoyote atakayekuwa analegalega katika kutekeleza wajibu wake wa msingi hasa katika kutatua changamoto na kuweka uwazi shughuli zinazohimiza jamii wanaioyongoza
"Tunaamini kwamba kazi mojawapo ya CCM ni kuondoa changamoto na kurahisisha maisha ya Mtanzania , kwa hiyo yule ambaye hayuko tayari kuendana na frika za CCM sisi hatuko tayari.
" Tutamshika mkono kiongozi ambaye anahangaika na mambo ambayo yanahusu watu ikiwemo kueleza uwazi wa shughuli zinazohimiza watu namna gani watatua changamoto hizo...
"Na namna gani anashirikiana nao lakini kuwapa uwazi kile ambacho amekikusanya na kikutumia katika kutatua changamoto za wananchi wa eneo husika, " amesema Gavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...