KAMPUNI inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi Maisha ya kidijitali, Tigo, leo imezindua kampeni mpya inayojulikana kama 'ChaWote' ambapo wateja watajishindia zawadi kambabe pale wanapofanya miamala kwa kutumia mtandao wa Tigo. Hii ni promosheni ya kipekee kwani kila mteja wa Tigo ni mshindi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni iyo Bi. Angelica Pesha Afisa Mkuu wa Tigo Pesa amesema
"Kampeni hii inawapa wateja nafasi ya kujishindia zawadi za fedha taslimu hadi TShs 5, 000, 0000 na bonasi za papo hapo za hadi dakika 100 na SMS 100 kwa siku 90 , Ili kuweza kuwa mshindi kwenye kampeni hii ya ChaWote, wateja wa Tigo wajinunulie vifurushi vyao pendwa vya siku, wiki na mwezi kupitia Tigo Pesa kwa kupiga *150*01# au Tigo Pesa App. Pia wateja wanapolipia huduma au bidhaa kupitia Lipa kwa Simu watapa bonus za papo hapo za Dakika na SMS na kuingia kwenye droo inayowapa nafasi ya kujishindia hadi TSh 1,000,000 kila siku na TSh 5,000,000 kila mwezi "
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...