Na.Damian Kunambi, Njombe

Baada ya kutolewa katazo la kutumia mazao yatokanayo na mnyama aina ya Nguruwe wilayani Ludewa mkoani Njombe ambalo lilitolewa kwa zaidi ya miezi miwili na nusu iliyopita kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na uwepo wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe hatimaye mnyama huyo ameweza kupunguziwa masharti ya katazo hilo baada ya kupungua kwa matukio ya ugonjwa huo.

Akizungumzia kufunguliwa huko Afisa Kilimo Mifugo na Uvuvi Festo Mkomba amesema mnyama huyo ameruhusiwa kuchinjwa pamoja na kutumika mazao yake kama nyama, mifupa, nywele, samadi na damu ila hairuhusiwi kutoa mazao hayo nje ya kijiji ambacho mnyama huyo amechinjwa ambapo na kabla ya kuchinjwa kwake anatakiwa kufanyiwa ukaguzi kwa masaa yasiyopungua 48.

"Tumeruhusu matumizi ya mnyama huyu lakini bado tunasisitiza wananchi kuwa na tahadhari kwa kuhakikisha nyama ama mazao watakayokuwa wanatumia ni salama na endapo watahisi nguruwe wao kuwa na dalili yoyote ya ugonjwa basi watoe taarifa kwa maofisa ugani ama katika ofisi za serikali ya kijiji ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa".

Ameongeza kuwa katika kipindi cha ugonjwa huo kwa Halmashauri hiyo pekee nguruwe zaidi ya 417 wamekufa kwa ugonjwa huo lakini walifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha ugonjwa huo hauenei zaidi na wamefanikiwa ambapo kwa sasa hakuna nguruwe hata mmoja mwenye ugonjwa.

Amesema kwa Wilaya hiyo maeneo ambayo yameonekana kuathiriwa zaidi na ugonjwa huo ni kata ya Mundindi, Lugarawa, Mavanga na Ruhuhu.

"Tumekuwa tukioa elimu na kupita kukagua nguruwe katika maeneo mabalimbali ya wilaya hii na tumefanikiwa kutokomeza ugonjwa huu japo haikuwa rahisi kwakuwa kuna baadhi ya watu wasio waaminifu walikuwa wakichinja kwa siri na kuuza nyama hiyo huku wakiwa wameipa jina la Mbolea ya Ruzuku ili wasigundulike kwa urahisi".

Sanjali na hilo pia Mkombe ameziomba taasisi mbalimbali binafsi na serikali kuchukua hatua katika kufanya utafiti wa dawa ama chanjo ya ugonjwa huo kwani umekuwa ukijirudia mara kwa mara na hasa katika ukanda wa nyanda za juu kusini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...