Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji ambazo zimetolewa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter zenye lengo la kuchafua biashara zake.

Mkurugenzi mtendaji wake Zulfikar Ismail amewaambia waandishi wa habari leo kuwa taarifa ambazo zimeandikwa kwenye mtandao na Twitter( akautaja) umedai ujenzi wa mradi wa hoteli ya kitalii Lake Magadi iliyoko ndani ya Hifadhi ya Serengeti kuwa haukufuata taratibu hazina ukweli wowote bali ni upotoshaji unaopaswa kupuuzwa.

"Taarifa zilizochapishwa kwenye mtandao huo wa kijamii kuanzia Mei 30, 2023 ni ya uongo na isiyo na utafiti wowote, na imekosa uhalali wa kuheshimiwa na kupokelewa na jamii kwani imejaa maneno ya kuokoteza barabarani ...

" Kampuni hii imekua ikifuata sheria katika utekelezaji wa miradi yake na kwa muda mrefu na imejijengea heshima kubwa kutokana na ubora wa hoteli zake hivyo haitakubali kuchafuliwa Kwa namna yoyote ile" imesema taarifa hiyo

Kuhusu ujenzi wa Loji/ Hoteli inayojengwa kwenye eneo la Magadi Serengeti taarifa hiyo imesema kuwa mradi huo umefuata hatua na taratibu zote za kisheria na kwa sasa iko hatua za mwisho kukamilika.Inatarajiwa kufunguliwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2024.

Mradi wa hotel hiyo ya Kitalii ya nyota Tano( five star hotel) ina idadi ya vyumba 75 na ina thamani ya Sh.bilioni 43.68 yenye uwezo wa kupokea wageni 150 Kwa wakati Mmoja.

Kuhusu manufaa ya mradi huo taarifa hiyo imesema ni pamoja na kutoa ajira Kwa wafanyakazi zaidi ya 180 wa Moja Kwa Moja , ajira zisizo za moja kwa moja kama vile kuuza bidhaa zao kwenye hoteli hiyo.

Pia ongezeko la watalii, kuchangia pato la Taifa Kwa kulipa kodi sambamba na utekelezaji Kwa vitendo dhana ya Royar Tour iliyofanywa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya Utalii hapa nchini.

Aidha kampuni ya Wellworth Hotels anda Lodges Ltd imeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji hapa nchini.

"Sisi kama wawekezaji wazawa wataendelea kushirikiana na serikali katika kuendelea kukuza biashara hapa nchini kupitia hotel zetu za kitalii." amesema.

Kupitia taarifa hiyo Kampuni hiyo imewaomba Watanzania wazidi kuinga mkono serikali ya Awamu ya sita nakuwapuuza wale maadui wachache wa maendeleo hapa nchini wakiwemo wale wanaotoa habari za kupotosha kwa lengo la kuwakatisha tamaa wawekezaji wazawa.

Hata hivyo taarifa ya kampuni hiyo ,Mei 31 2023 Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisa Uhifadhi Mwandamizi Kitengo Cha Mawasiliano Catherine Mbena imesema Kampuni ya Wellworth Hotels and Lodges Ltd ilipewa eneo la ujenzi wa Loji katika eneo la ziwa magadi Serengeti mwaka 2015 ,kwa barua kumb.Na.TNP/HQ/P.30/17 ya tarehe 04/06/2015 ,

Kwa mujibu wa taarifa ya TANAPA mwekezaji huyo alikamilisha taratibu zote ndani ya shirika pamoja na Baraza la Uhifadhi na Usimamaizi wa Mazingira (NEMC) inayomtaka mwekezaji kufanya tathmin za athari za kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa loji ndani ya hifadhi ambapo ulikamilika na kupewa cheti cha Mazingira namba EC/EIS/2435 cha tarehe 16/05/2016.

TANAPA imesema kutolewa kwa cheti cha mazingira kwa undelezaji wa eneo hilo la uwekezaji linakidhi vigezo vya kuendeleza nakuongeza kuwa ujenzi wa Loji hiyo ulianza mwaka 2017 na kuendelea hadi mwaka 2018.Ujenzi ulisimama kutokana na la UVIKO 19 na mwaka 2021 kazi ya ujenzi wa huo iliendelea tena.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...