Na Said Mwishehe, Michuzi TV –Butiama

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Wilaya ya Butiama mkoani Mara umesema umeendelea na jitihada za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere katika masuala ya uihifadhi na utunzaji mazingira kwa kutoa elimu kwa wananchi kutambua umuhimu wa utunzaji mazingira .

Aidha mbali ya uhifadhi na utunzaji mazingira, TFS wilayani Butiama wanajihusisha na shughuli za ufugaji nyuki katika hifadhi ya msitu wa Kyarano
Iliyoanzishwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1983 kwa lengo la kuhifadhi bwawa la maji ambalo alichimba kwa mikono yake kwa kushirikiana na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara ya kutembelea hifadhi ya Kyarano kwa lengo la kuona shughuli za uhifadhi, Mhifadhi Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Hafidh Said amesema kwa Wilaya ya Butiama wwmejitahidi kuhifadhi mazingira kwa kuelimisha wananchi jinsi ya kutunza mazingira na ufugaji nyuki.

"Katika hifadhi yetu hii TFS tumeendelea kutunza mazingira lakini tunaendelea na ufugaji nyuki ndani ya hifadhi hii, kwa sasa tunayo mizinga 180 na kati ya hiyo mizinga 40 ni ya kibiashara na huu ni msimu wa kuvuna asali, " amesema Mhifadh Said.

Akifafanua zaidi shughuli zinazofanywa na TFS Wilaya ya Butiama , Mhifadhi huyo amesema wamekuwa wakitoa kuhusu masuala ya uhifadhi, kuhamasisha ufugaji nyuki katika eneo la Kyarala na Kianyari ambako wanahamasisha watu kufuga nyuki na kuachana na tabia ya kukata miti na kuchoma mikaa.

"Shughuli nyingine tunayoifanya hapa Butiama tunapanda miche na tunasisitiza wadau wanaoweza kuotesha miche waje kupata tunatoa elimu ya utoshaji miche.Pia tunagawa miche ya miti bure na kwa mwaka huu tumeshagawa miche 150,000, " amesema.

Kuhusu Mwalimu Nyerere na uihifadhi amesema katika Taifa la Tanzania Nyerere ni muasisi wa uhifadhi, ukiangalia hifadhi nyingi yeye ndio alianzisha licha ya wakoloni nao kuwa walikuww wameanzisha baadhi ha hifadhi lakini hifadhi nyingi Mwalimu Nyerere ndio ameanzisha na wilayani Butiama katika eneo lake la Mwitongo kuna hifadhi inaitwa Mwitongo ambayo yeye alianzisha

Akielezea zaidi kwa hifadhi ya Kyarano pia Mwalimu Nyerere ndio alianzisha na lengo kubwa ilikuwa ni kuhifadhi bwawa lililochimbwa kwa mikono ili lihifadhiwe, hivyo kwa mwalimu ni muasisi namba moja kwenye uhifadhi lakini hata viongozi ambao wamemfuata nao wamekuwa wakifuata nyayo zake katika suala la uhifadhi na utunzaji mazingira.

"Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akifuata nyayo za Mwalimu Nyerere, kwa mfano sasa hivi tunayo maelekezo kwa kila wilaya angalau tupande miche milioni moja, kwa hiyo ni sehemu ya jitihada ambazo anazionesha katika uhifadhi ili kuepuka athari za kimazingira kama mabadiliko ya tabianchi, " amesema na kusisitiza Rais Samia Suluhu Hassan anafanya jitihada kubwa za kufanya nchi iwe ya kijani.

Pamoja na hayo amesema TFS Wilaya ya Butiama wanajivunia uelewa wa wananchi ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira, ni watu wenye uelewa mkubwa kuhusu uhifadhi na ndio maana hata wanapoambiwa wasiharibu mazingira wanasikiliza na kufuata.

Kwa upande wake Ofisa Nyuki Wilaya ya Butiama Adam Machibya ameendelea kuwahamasisha wananchi hasa vijana kujihusisha na ufugaji nyuki kwani una faida nyingi ikiwemo ya kujiongezea kipato kutokana na mazao ya nyuki kama asali na nta.

"Butiama watu wamehamasika na tayari kuna vikundi 12 ambavyo vinajihusisha na ufugaji nyuki, wote wanazalisha ijapokuwa kuna baadhi ya vikundi wameanza mwaka huu hivyo bado hawajaanza kuvuna, vikundi hivyo vinafadhiliwa na TAFORI.

" Vijana wa Butiama wanatakiwa kujiingiza katika ufugaji nyuki kwasababu hata ukiangalia na mazingira yetu yanahamasisha kutokana na uwepo wa mvua za mara kwa mara hususani zinaanza Septemba mpaka Juni, kwa hiyo ni rahisi kwao kufuga na kupata mazao ya nyuki.

"Pia ni rahisi kupata makundi ya nyuki kwasababu ni wengi,unaweza kutundika mzinga leo na ukakaa siku mbili nyuki wakaingia na kinachovutia nyuki kukaa eneo fulani ni maua na maji na kwa Wilaya ya Butiama maua ni mengi hivyo nyuki wanapenda kuwepo, " amesema.

Ofisa Nyuki wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Wilaya ya Butiama Adam Machibya akielezea namna ya nyuki wanavyofugwa na faida zake
Mhifadhi Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Hafidh Said akielezea jitihada wanazofanya katika utunzaji mazingira sambamba na ufugaji nyuki unaofanyika ndani ya hifadhi ya Msitu wa Kyarano uliopo wilayani Bunda mkoani Mara
 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...