Makamu Mwenyekiti  wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema CCM ndiyo chama kinachofaa kuongoza Zanzibar.

Amewahimiza umoja na mshikamano kwa wanachama wa CCM kujiandaa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025.

Ameyasema hayo leo tarehe 11 Juni 2023  ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa akizungumza na Viongozi wa CCM ngazi ya Shina,  Wajumbe wa Halmashauri Jimbo, Wilaya na Mkoa huo.

Makamu Mwenyekiti Dk.Mwinyi  amewataka wana CCM kuvunja makundi, watakaoendeleza kuchukuliwa hatua na kamati za maadili za CCM .

Vilevile ametoa rai kufanyika kwa mafunzo ya itikadi kwa ngazi zote kwa Viongozi wa CCM pamoja na kuhimiza kuendelea kufanyika vikao vya kikatiba katika kila ngazi.

🗓️11 Juni 2023

📍Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...