Mratibu wa Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) Iliyoboreshwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam Yassin Kisawike akizungumza waandishi wa habari kuhusiana na waajiri wa kampuni mbalimbali kuwaunganisha wafanyakazi Mfuko wa  Afya ya Jamii (CHF) wakati wa Mkutano wa wadau wa kampuni mbalimbali, Jijini Dar es Salaam.
Afisa Rasilimali Watu wa Kamal Steel Limited Evanice Matemba akizungumza kuhusiana na CHF katika kwenda kupeleka taarifa kwa uongozi wa juu kwa wafanyakazi kukatiwa CHF , jijini Dar es Salaam.
Meneja Rasilimali  Watu wa Kampuni ya TLA Printing and Package Joseph Mabanga akizungumza umuhimu bima ya CHF kwa wafanyakazi katika mkutano wa Wadau jijini Dar es Salaam.

*Wadai rahisi kwao katika kuhudumia wafanyakazi wao katika kuimarisha Rasilimali Watu.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WAAJIRI wa Kampuni na Viwanda katika Mkoa wa Dar es Salaam waaswa kuwaunganiisaha wafanyakazi wao katika Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii Iliyoboreshwa (CHF) ili kutoa urahisi wa upatikanaji wa huduma bora za Afya na kwa gharama nafuu.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) Iliyoboreshwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam Yassin Kisawike katika mkutano na maafisa rasilimali wa kampuni mbalimbali ambapo amesema huduma ya mfuko huo inapatikana kila Halmashauri Jijini Dar es Salaam na wanalenga kupanua wigo zaidi wa utoaji huduma hiyo.

Aidha amesema kuwa kwa Dar es Salaam bado kuna watu wanaofanya katika viwanda na bado hawana bima hiyo ambayo kwa mtu mmoja ni shilingi 40,000 familia nishilingi 150,000 hivyo ni wakati sasa waajiri kuhakikisha wanawaunga wafanyakazi wao katika Mfuko huo ili wawe wachapakazi na wajenzi wa Taifa.

“Bima ya Afya ya Jamii inatoa fao la matibabu kwa wanachama, na Mwanachama wa Bima ya CHF iliyoboresha anaweza kuwa mtu binafsi au familia ya watu wasiozidi 6 kwa maana ya mkuu wa kaya na wategemezi wake” Amesema Bw. Kissawike.

Hata hivyo amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam hadi sasa waliojiunga na mfuko huo ni asilimia 11 tu ya watu zaidi ya milioni tano hivyo idadi bado ni ndogo na wanaendelea kufanya uhamasishaji ili waongeze wanufaika na wanachama wa mfuko huo na idadi itakapo kuwa kubwa na huduma itakuwa bora zaidi.

Sambamba na hayo amesema changamoto inayosababisha idadi ndogo ya wanachama ni uelewa mdogo kwa jamii kuhusu bima na pia ni hiari hivyo haoni sababu ya kujiunga na bima.

“Jamii bado ina maswali mengi inajiuliza kwa nini wajiunge na bima wakati hawaumwi mara kwa mara , ila niishauri jamii kuwa bima inapunguza gharama za matibabu hususani pale ugonjwa au ajali inapotokea ghafla”Ameongeza Kisawike.

Kwa upande wake Meneja Rasilimali watu toka Kampuni ya TLA Printing and Package Joseph Mabanga amesema uwepo wa bima ya Afya unawafanya wafanye kazi kwa kujiamini na pia wafanyakazi wanakuwa na uhakika wa matibabu yao na familia zao.

Aidha amesema kuwa uhakika wa matibabu kupitia Bima ya afya ya jamii ya CHF iliyoboreshwa inafaida kwa mtu moja, familia na taifa kwa ujumla hivyo watanzania wajiunge na bima hiyo.

Mkutano huo uliandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwakushirikiana na Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...