Mtoa mada na mwanasheria wa Takukuru, Bw. Imani Mizizi akizungumza wakati wa mafunzo ya juu ya Rushwa mahala pa Kazi kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Juni 02, 2023.

 Kaimu RASI wa ndaki Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe na Mhadhiri mwandamizi wa masomo ya uchumi, Coletha Komba akifungua mafunzo juu ya Rushwa Mahala pa kazi kwa niaba ya RASI wa Ndaki hiyo, Profesa Cyriacus Binamungu yaliyotolewa leo Juni 02, 2023 katika Ndaki hiyo kwa Wafanyakazi wote.
Mhadhiri mwandamizi wa masomo ya Sheria chuo Kikii Mzumbe , Ndaki ya Dar es Salam, Norah Msuya akizungumza wakati wa mafunzo juu ya Rushwa Mahala pa kazi  leo Juni 02, 2023 katika Ndaki hiyo kwa Wafanyakazi wote.

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Juni 02, 2023 mara baada ya mafunzo ya juu ya Rushwa mahala pa Kazi yaliyotolewa na Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania.

Mtoa mada na mwanasheria wa Takukuru, Bw. Imani Mizizi akizungumza wakati wa mafunzo ya juu ya Rushwa mahala pa Kazi kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Juni 02, 2023
upande wa Mwanasheria kutoka TAKUKURU, Fatuma Waziri akizungumza wakati wa mafunzo ya juu ya Rushwa mahala pa Kazi kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Juni 02, 2023.


Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakichangia mada leo Juni 02, 2023 wakati wa mafunzo ya juu ya Rushwa mahala pa Kazi.

Matukio mbalimbali.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) watoa elimu juu ya rushwa Mahala pa kazi kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Juni 2, 2023.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo mtoa mada na mwanasheria wa Takukuru, Bw. Imani Mizizi ametaja sababu mbalimbali za kuwepo kwa rushwa katika vyuo kuwa ni ushawishi wa watu wenye mamlaka pamoja na uwepo wa mifumo dhaifu ya kushughulikia rushwa ya ngono mahala pa kazi.

Ameongeza kuwa sababu nyingine ni aibu na woga wa kutoa taarifa kwa waanga wa rushwa ya ngono ingawa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 imetamka kosa la ruswa chini ya kifungu ch 25 hivyo ni kosa kisheria.

“Mtu yeyote mwenye mamlaka katika kutekeleza majukumu yake anadai au anaweka sharti la ngono au upendeleo mwingine wowote kama kigezo cha kutoa ajira, kupandisha cheo, kutoa haki au upendeleo wowote unaotambulika kisheria atakuwa ametenda kosa.” Sheria ya Rushwa ya ngono inavyoeleza alisisitiza Bw. Mizizi.

Awali Mizizi alieleza maana ya rushwa ya ngono na kueleza kuwa vitendo vya ngono ni kujamiiana na mwanaume na mwanamke, ngono za jinsia moja nayo ikatamkwa mara kwa mara huku matendo yote hayo yakitafsiliwa kuwa ni rushwa.

Kwa upande wa Mwanasheria kutoka TAKUKURU, Fatuma Waziri amesema kuwa ifike mahala kila mmoja katika vitengo vyote asimamie sheria, taratibu na kuzingatia kanuni za utawala bora ili kuweza kundoa aina zote za rushwa Mahala pa Kazi.

Bi. Fatuma ameeleza kuwa ukosefu wa utashi wa kuzuia na kupambana na rushwa nayo imeelezwa kuwa ni sababu za kuwepo kwa rushwa mahala pa kazi.Ameongeza kuwa kuna wa imani potofu kuwa rushwa ni ujanja, upendeleo au njia ya mkato kupata haki na kuoneana aibu, huu ni uvunjaji wa sheria.

Akizungumzia kuhusiana na mafunzo hayo, Naibu Mshauri wa Wanafunzi, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam zitta Mnyanyi amesema kuwa mafunzo ni mkakati wa chuo ili kuhakikisha kuwa Rushwa inazuiliwa kuanzia ngazi ya chini kuanzia pale ambapo mwanafunzi anafika chuoni ili kusije tokea matukio ya utovu wa nidhamu kwa ajili ya kutafuta haki ambayo ni lazima upewe bila kutoa chochote.

“Suala la Rushwa ni suala mtambuka na hasa kwenye taasisi zetu hizi ni suala ambalo halikwepeki wala huwezi kusema havipo.”Akitolea mfano Zitta amesema kuwa kuna maeneo matatu yanaleta shida ya rushwa katika Taasisi za elimu ambazo ni rushwa ya ngono, rushwa ya upendeleo na rushwa ya pesa.”

Pia Zita ametoa wito kwa wafanyakazi kama wanatabia ya kutoa au kuomba rushwa mahala pa kazi kuacha kwani inaleta athari ki elimu kwa sababu kama mwanafunzi akiwa na tabia ya kutoa rushwa hataweza kuihudumia jamii hapo baadae atakapo pata nafasi ya kuhudumia.

Kwa upande Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Faisal Issa amesema mafunzo hayo yanamanufaa makubwa kwani ni muhimu kuzingatia kwani suala la Rushwa linaondoa haki kwani haki ni jambo la msingi na la muhimu kwa jamii hasa taasisi za elimu.

“Chuo kiandae mafunzo hayo mara kwa mara inatokea nafasi ili kuweza kuwakumbusha wafanyakazi suala zima kuhusu rushwa hata kwenye nyumba za ibada inahubiriwa waumini kutenda mema lakini mabaya yahajawahi kuisha popote hivyo mafunzo hayo ya rushwa mahala pa kazi iwe ni kwa kila mara ili kuweza kukumbushana”

Dkt. Issa ameshauri wanafunzi kusoma kwa bidii na kufuata sheria na miongozo ya chuo ili kuepuka kuingia katika kutoa au kupokea rushwa kwani hakuna njia ya mkato ya kufanisha jambo zaidi ya kuzingatia masomo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...