Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Chato

WATUMISHI wa Shamba la Miti Silayo wilayani Chato mkoani Geita wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa nyumba za watumishi ambazo zimejengwa katika shamba hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Msaidizi wa Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Silayo ambalo liko chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mhifadhi Patrick Mbugi amesema kwa Serikali pamoja na TFS wameona haja ya kujenga nyumba za watumishi katika shamba hilo.

“Ili watumishi waweze kufanya kazi vizuri ni vema wakawa na mazingira mazuri ya kiutendaji, kutokana na umuhimu huo tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutujengea makazi ya watumishi wa shamba la miti silayo .

“Watumishi wanakaa kwenye nyumba nzuri na mazingira bora, hivyo mazingira mazuri husababisha hata ufanisi katika utendaji wetu wa kila siku kuongezeka.Pia tunahukuru kwa kujengewa ofisi kubwa, nzuri na ya kisasa ndani ya shamba hili,”amesema Mbugi.

Kwa upande wake Askari Mhifadhi wa Shamba la Miti Silayo amesema kwamba wanaishukuru Serikali ya Rais Dk.Samia kwa ujenzi wa makazi ya watumishi wa shamba hilo.

"Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mama shupavu kwa ujenzi wa makazi haya mazuri kwa ajili yetu, hakika uwepo wa nyumba karibu na eneo letu la kazi imeturahisishia sana na kubwa zaidi tumepunguza gharama za nauli lakini pamoja na kodi za nyumba kwa kupanga maeneo ya mjini, " amesema Mollel.

Wakati huo huo katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila Juni 5 ya kila mwaka, Shamba la Miti Silayo wamesema wanaungana na serikali kuadhimisha siku hiyo na kwa upande wao wanaendelea kuhamasisha kuhamasisha jamii kupanda miti kwenye maeneo yao.

Pia wameendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wapate uelewa na kuwa na muitikio chanya katika utunzaji mazingira sambamba na kukumbusha umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji.

Mhifadhi Patrick Mbugi ambaye pia ni Msaidizi wa Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Silayo akielezea umuhimu wa nyumba ambazo zimejengwa na Serikali kwa ajili ya kuwawezesha watumishi wa shamba hilo kuwa na makazi
Muonekano wa baadhi ya nyumba ambazo zimejengwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kwa ajili ya watumishi wa Shamba la Miti Silayo lililopo wilayani Chato mkoani Geita.Nyumba hizo zimejengwa katika shamba hilo na hivyo kuwawezesha watumishi kuwa karibu na maeneo yao ya kazi.

Askari Mhifadhi wa Shamba la Miti Silayo Juliana Mollel akizungumza na waandishi alipokuwa akitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea nyumba watumishi wa shamba hilo na hivyo kuwaondolea gharama za nauli na kodi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...