CHAMA Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni kimeendelea kumwagia sifa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa mbali na kuipenda sana Wilaya hiyo lakini wanampongeza zaidi kwa mchakato wa kushughulikia suala la Bandari.
Kadharika, Wilaya hiyo imesema pia kutokana na kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt. Samia kwenye Nchi na kwenye Wilaya hiyo wanamuomba kwa suala la Bandari basi aendelee nalo tena kwa kasi kubwa na wala asiyumbishwe na mtu yeyote.
Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Wilaya hiyo Shaweji Mkumburwa wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi na kusema kuwa Bandari ni kitu muhimu zaidi na kwamba Kinondoni iko naye kwa hali na mali na itaendelea kumpa ushirikiano mkubwa.
"Ninayasema haya anayotufanyia Rais Wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan (Shujaa wetu) kwani mbali na hayo pia tumepata Mradi wa DMDP wa Barabara ambapo kila Kata inauwezo wa kupata alau barabara moja ambapo ni sawa na Kilometa 57 sawa na asilimia 30," alisema Mwenyekiti na kuongeza;

"Hivyo bado kuna asilimia 70 tukizipata tutapata barabara kwa asilimia zote lakini pia nasifu ushirikiano ninaopewa na viongozi walioteuliwa na Rais Dkt. Samia lakini pia nawapongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mkurugenzi na viongozi wengine,".
Alisema wanakinondoni wanampenda sana Rais Samia (Shujaa) na wataendelea kumuunga mkono kwa hali na mali katika utekelezaji wa majukumu yake.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi ujao Mwenyekiti Mkumburwa, alisema kuwa wamejipanga vizuri kwani wamewambia Kata na kwenye Matawi ifikapo Agasti 31, mwaka huu kila nafasi iwe imekamilika ambazo watu hawapo.
"Awali tulifanya ziara kuweka mambo sawa katika Kata na kwenye Matawi hivyo ninawahakikishia Kinondoni iko salama kwa kuongeza idadi ya wanachama kwani bado ni wachache na sisi tunataka ifikapo Desemba tuwe na wanachama 500,000 (laki tano).
Alisema pia Wilaya imewahimiza Wenyeviti na viongozi wengine kuubili mshikamano, kutatua na kusikiliza kero za wananchi na kwamba hawakuishia hapo bali imeagiza wabunge, madiwanina wenyeviti kushuka chini kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...