Na Mwandishi Wetu, Same
MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa Vijiji vitatu vya Tae, Mahande na Heikondi vilivyo kata ya Tae wilayani humo kushirikiana kuteketeza mashamba yote ya Mirungi na kuachana na zao hilo haramu.
Ameagiza viongozi wa Halmashauri kusimamia utekelezaji huo na kutumia wataalam wa Idara ya Kilimo kufanya utafiti na kuainisha mazao mbadala yanayostawi katika eneo hilo, na kutoa elimu kwa wananchi waweze kunufaika.
Mkuu wa Wilaya Mgeni ameyasema hayo leo Julai 11, 2023 katika mkutano wa hadhara maalum uliokuwa unalenga kuzungumzia kazi ya utekelezaji wa kuteketeza mashamba ya mirungi linaloongozwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya wakishirikiana na vyombo vingine vya Usalama.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)Aretas Lyimo amesema oparesheni hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani ambapo wamefanikiwa kuteketeza ekari 535 katika vijiji hivyo vitatu ndani ya siku saba.
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza na wananchi alipokuwa akitoa maelekezo ya mashamba yote ya mirungi kuteketezwa wilayani humo
Kamishina Jenerali qa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo akifafanua jambo kwa wananchi baada ya kufanyika kwa operesheni ya siku saba ambayo imewezesha ekari 535 za mirungi kuteketezwa katika baadhi ya vijijini wilayani humo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...