MKUU wa Wilaya ya Temeke Mhe. Mobhare Matinyi amwakilisha Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kumpokea Waziri Mkuu wa Burundi, Gervais Ndirakobuca, leo Julai 24 majira ya saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa nchi za Afrika wanakusanyika Jijini Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano wa Afrika wa Rasilimali Watu unaofanyika kwa siku mbili Julai 25-26 , 2023. Mwenyeji wa mkutano huo ni Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...