Na. Damian Kunambi, Njombe

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amewataka watendaji wa vijiji kutowachangisha wananchi michango ya maendeleo zaidi ya asilimia 20 katika miradi ile ambayo fedha zake hazijitoshelezi na kwa miradi ambayo serikali imetoa fedha asilimia 100 za kukamilisha miradi mizima kutowachangisha kabisa.

Mbunge huyo ameyasema hayo alipofanya mikutano katika vijiji vya Shaurimoyo, Mdilidili pamoja na Lugarawa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vijiji vyote vya jimbo hilo akiwa ameongozana na viongozi wa chama cha mapinduzi pamoja na wakuu wa idara wa halmashauri ya Ludewa kwa lengo la kutoa mrejesho na kusikiliza changamoto ambapo mpaka sasa tayari amekwisha tembelea vijiji 30 kati ya 77 vya jimbo hilo.

" Wananchi hawa wana vipato vya kawaida sana, kuwachangisha fedha kwa kila mradi ni kama mnawaonea hivyo niwaombe sana watendaji wangu kuwahurumia hawa wananchi, msiwabebeshe mizigo mingi hata ambayo serikali imewasaidia", Amesema Kamonga.

Kauli hiyo imekuja baada ya wananchi hao kutoa malalamiko mbele ya mbunge huyo juu ya michango hiyo na kudai kuwa kila mwaka wamekuwa wakichangia fedha za kuendeleza miradi ilihali serikali imekwisha toa fedha za miradi hiyo na endapo wakishindwa kuchangia hukamatwa na askari mgambo.

Josaya Luoga ni katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi wilayani humo aliwataka viongozi wa ngazi ya vijiji na kata kuwa waadilifu kwani idadi ya nguvu kazi zinazotajwa zimeonekana kutokuwa halisi ukilinganisha na wingi wa watu ambao ni nguvu kazi.

" Kuna kitu hakipo sawa hapa, kumekuwa na makadilio ya takwimu za nguvu kazi na kibaya zaidi kila mahali unakuta wanasema nguvu kazi ni 502, 504 yaani kila mtu ni miatano na kidogo kitu ambacho hakiwezekani kwani tukiangalia kwa idadi ya watu waliopo hapa tayari ni zaidi ya 500 pitieni upya takwimu zenu" Amesema Luoga.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...