Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, ametembelea na kukaa kutoa elimu kuhusu Utalii huku akiwaongoza pia mamia ya wananchi katika maonesho ya 47 ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam kufanya “Royal Tour” kwa kutembela vivutio mbalimbali vya utalii wakiwemo wanyama na vituo vya kuzalisha asali.

Akiwa kwenye Banda la awizara hiyo, Dkt. Abbasi amepata fursa ya kuwahudumia wananchi na kujibu swali la mmoja wa wananchi aliyetaka kujua hatua zinazochukukiwa na Wizara hiyo kulinda raslimali zilizoko chini ya dhamana yao.

Dkt. Abbasi alisema moja ya hatua kubwa ni kuunda Jeshi la Uhifadhi, ambako linapewa mafunzo na vifaa na kwa sasa limepata mafanikio makubwa katika kupambana na ujangili uliokithiri miaka ya nyuma na sasa wanyama wameongezeka.

“Chini ya Jeshi la Uhifadhi, maliasili zetu ziko salama zaidi sasa kuliko nyuma zilipokuwa chini ya maafisa tu wanyamapori ambao hawakuwa na silaha wala vifaa vya kuwalinda kisayansi zaidi,” alisema.

Akijibu swali kuhusu mafanikio ya Royal Tour, Dkt. Abbasi amesema filamu hiyo ineleta mafuriko ya watalii na kudokeza kuwa kwa namba za watalii zinavyokwenda huenda mwaka huu kufikia Disemba, lengo la Ilani ya CCM la watalii milioni 5 ifikapo 2025, litafikiwa miaka miwili kabla.

“Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan alipofanya Royal Tour alituagiza sote kupenda kutalii na leo nafurahi kuona mamia ya wananchi wanatalii hapa Saba Saba kwa kuona wanyama na vivutio vingine vya historia na utamaduni, lakini kwa ujumla Royal Tour imeleta mafuriko makubwa ya watalii na mpaka nusu mwaka Juni mwaka huu tumevunja rekodi za miaka yote ya nyuma kwa idadi ya watalii.

“Tunatarajia mwezi huu Julai Waziri wetu Mhe. Mohammed Mchengerwa atafanya mkutano mkubwa na wanahabari wa ndani na nje ya nchi kueleza rekodi hii,”alidokeza Dkt. Abbasi.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...