Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Geita Gold FC ya Tanzania inatarajiwa kusafiri nchini Rwanda Agosti 4 mwaka huu kwa ajili ya kambi maalum ya kujiandaa na msimu mpya wa mashindano wa 2023-2024 ambao unatarajiwa kuanza 15 Agosti, 2023.


Ikiwa nchini Rwanda, Geita Gold FC itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Mukura Victory FC ya nchini humo, Agosti 5, 2023 ikiwa ni mchezo wa kusherehesha sherehe za miaka 60 ya uhuru wa nchi hiyo.


Kabla ya kusafiri nchini Rwanda, Geita Gold itaanza kambi yake nyumbani nchini Tanzania, mkoani Morogoro kuanzia Julai 18, 2023 na watafanya mazoezi yao mkoani hapo na Julai 28 watacheza mchezo wao wa kwanza wa kirafiki.


Julai 29 hadi Agosti 2 mwaka huu, Geita Gold FCwataendelea na kambi yao mkoani hapo Morogoro katika mashindano mafupi yatakayofanyika katika dimba la Jamhuri. Agosti 3 watarejea mjini Geita kwa ajili ya maandalizi ya safari ya Rwanda, safari itakuwa Agosti 4 mwaka huu.


Geita Gold FC wakiwa nyumbani mjini Geita watazindua Jezi zao mpya za msimu ujao na wataipongeza timu yao ya vijana ya  U-20 ambao iliibuka nafasi ya pili katika mashindano ya vijana yaliyofanyika mwaka huu katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini na Mtibwa Sugar (U-20) waliibuka vinara.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...