Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV- Kigoma
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Daniel Chongolo amesema Chama hicho
kinaelekeza Serikali kuisukuma na kuongeza spidi katika kuhakikisha
mjadala wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam unafika mwisho ili
wananchi waanze kuona matokeo yake.
Chongolo ameyasema hayo leo
Julai 26,2023 wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kigoma kupitia
mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mwanga Center ambapo ametumia
nafasi hiyo kuitaka Serikali isiingie kwenye maneno ya siasa na badala
yake wasimame kwenye hoja na hatimaye bandari iongeze ufanisi.
"Tunanachotaka
ni kuona bandari inaongeza ufanisi,inaletea matokeo na inachangia pato
kubwa la Taifa na kuongeza tija kwa nchi ya kuwahudumia Wananchi na sio
vinginevyo.Mambo yote ya maneno maneno,siasa hizi tusizipe nafasi.
"
Sisi ndio tumepewa dhamana ya siasa,sisi tunakuja kuzungumza na
wanasiasa wenzetu na Watanzania waliotupa dhamana,Serikali mambo yao ni
ya kutenda na kuleta matokeo,na wasifanye mchezo hata kidogo kutosimamia
maslahi ya nchi kwa kila wanachokifanya’’,amesema Chongolo.
Aidha
Chongolo alieleza hatua kwa hatua kuhusu uamuzi wa Serikali kuingia
makubaliano ya uwekezaji wa kuboresha uendeshaji wa Bandari ya Dar es
Salaam huku akifafanua lengo kuu ni kuhakikisha bandari hiyo inatoa
huduma kwa ufanisi mkubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...